Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, July 19, 2013

WAHARIRI LAWAMANI MASLAHI DUNI YA WAANDISHI WA HABARI

WAHARIRI wa habari katika vyombo mbalimbali nchini wametajwa kuwa miongoni mwa watu wanaochangia kwa kiasi kikubwa waandishi wa habari wa kawaida kuwa na maslahi duni. Hayo yamebainishwa na wajumbe wa Balaza la katiba la Tasnia ya Habari waliohudhuria warsha ya siku moja ya kujadili rasimu ya katiba mpya iliyofanyika jijini Mbeya ni ya nne baada ya zilizofanyika Zanzibar,Dar es salaam na Mwanza. Wajumbe hao walipendekeza katiba ijayo izingatie sheria itakayowezesha wanahabari kunufaika na jasho la kazi yao tofauti na ilivyo hivi sasa. Mmoja wa wajumbe wa balaza hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa,Frank Leonard alisema kwa muda mrefu wamiliki wa vyombo vya habari wamekuwa wakitupiwa lawama juu ya maslahi duni kwa waandishi wa vyombo vyao mzigo ambao kiukweli si wa kwao. Leonard alisema tatizo lililopo ni bodi za wahariri za vyombo husika kusahau majukumu yake ya kuwa kiunganishi kizuri baina ya mmiliki wa chombo na mwandishi wa kawaida badala yake bodi hizo zimekuwa zikiwajali wahariri pekee na kuwaeka waandishi kama watu wa kutumika. “Ukifuatilia kwa undani utakuta mmiliki wa chombo husika hajui nini kinaendelea.Anajua kila mmoja anapata kile anachostahili.Hii ni kwakuwa kiunganishi ambacho ni mhariri hajafanya kazi yake.Ni vema sasa katika katiba ijayo waandioshi na wao wakaanza kunufaika na jasho lao” “Kwa muda wa zaidi ya miaka sita tumekuwa tukipigania mambo matatu.Sheria ya vyombo vya habari,Uhuru wa habari na Uhuru wa kujieleza.Uhuru wa kujieleza umekua kwa sasa lakini si kwa kiwango tunachohitaji bado kuna tatizo” Mjumbe mwingine kutoka mkoani Rukwa Samii Jumaa Kisika aliwataka wanahabari kulitumia balaza la katiba la tasnia ya habari kutoa mapendekezo yatakayowezesha kunufaika na shughuli yao kuliko ilivyo hivi sasa. Kisika alisema ni vema wanahabari wakaanza kujitetea wenyewe badala ya kuendelea kupigia kelele maslahi ya wengine wakati wao wananyongwa kila siku na hawasemi.

No comments:

Post a Comment