Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, July 5, 2013

7 MBARONI KWA KUCHOMA NYUMBA MOTO

MNAMO TAREHE 04.07.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILUNGU – IZIWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALICHOMA MOTO NYUMBA YA MUSA S/O KEYA,MIAKA 35,MSAFWA,MKULIMA ,MKAZI WA IZIWA ILIYOJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA KWA KUTUMIA NYASI NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA NYUMBA HIYO. CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA BAADA YA WANANCHI KUMTUHUMU KAKA WA MHANGA SAMSON S/O KEYA,MIAKA 60,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA ILUNGU AMBAYE ALIKUWA AMEJIFICHA NDANI YA NYUMBA HIYO KUWA NI MCHAWI NA AMEMLOGA MAREHEMU ESTER W/O MUSA MKE WA MHANGA . HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA KWANI SAMSON S/O KEYA ALIFANIKIWA KUTOKA NDANI YA NYUMBA HIYO NA KUKIMBIA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA KWA MOTO BADO KUFAHAMIKA. KUFUATIA TUKIO HILO WATU SABA WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO AMBAO NI 1.YOHANA S/O SOLOMONI, MIAKA 38,MSAFWA,MKULIMA 2.TUMAINI S/O ANTHON,MIAKA 25,MSAFWA,MKULIMA 3.MOSHI S/O GEORGE,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA .4. DAUD S/O LINGI,MIAKA 25,MKULIMA,MSAFWA , 5.MUSA S/O PHILIPO,MIAKA 36,MSAFWA,MKULIMA ,6.TAMSON S/O GWILAJE,MIAKA 27,MSAFWA NA 7. LASTON S/O MBALAMWEZI,MIAKA 52, MKULIMA ,MSAFWA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ILUNGU-IZIWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI . KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINARUDISHA NYUMA MAENDELEO. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WATU WENGINE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

No comments:

Post a Comment