Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 22, 2013

PINDA KUZINDUA UTOAJI VYETI VYA KUZALIWA MBEYA KESHO

WAKAZI mkoani hapa hususani katika jiji la Mbeya wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye uzinduzi wa utoaji vyeti vya kuzaliwa utakaofanyika kesho(Julai 25) kwenye viwanja vya Luandanzovwe vilivyopo eneo la CCM jijini humo. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa hamasa hiyo na kubainisha kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo ambao hafra yake itaanza majira ya asubuhi. Mpango huo wa utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa wakazi utawezesha upatikanaji wa urahisi wa vyeti hivyo tofauti na awali kwakuwa kwa sasa wananchi watajipatia vyeti hivyo kupitia ofisi za kata wanazoishi badala ya ofisi za makatibu tawala wa wilaya. Tayari ofisi ya Usajili wa Vizazi na vifo(Rita) inayohusika na utoaji vyeti hivyo imekwishatumia mitandao mbalimbali ikiwemu simu za mikononi kutuma ujumbe unaotoa maelekezo ni kwa namna gani wakazi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano watapata vyeti vyao kuanzia Julai 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment