Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 22, 2013

CHADEMA WAZIDI KUCHAFUA HALI YA HEWA.WATUMIA MKUTANO WA MBEYA KUSISITIZA RED BRIGED

PAMOJA a kupigwa mkwara mzito na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa juu ya mpango huo na kutishiwa kufutiwa usajiri,chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesisitiza nia yake ya kuwa na jeshi lake kinaloliita vijana wakakamavu ama Red Brigedi. Jana Chadema kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami kwa vijana wao maarufu kama Red brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka huu. Kiongozi wa ulinzi wa chama hicho kanda ya Nyanda za juu kusini Lucas Mwampiki ametangaza tarehe ya kuanza mafunzo hayo kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Mbalizi wilayani Mbeya na kubainisha kuwa ameamua kuweka wazi adhima hiyo ili serikali isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa kuwazuia. “Polisi msisumbuke kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa nane mwaka huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete Jijini Mbeya. Mgeni rasmi katika mkutano huo Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na Mbunge wa Arusha mjini, alisema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na kuachwa bila ajira ili wajiunge na mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment