Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, July 7, 2013

FAMILY DAY YA TBL MBEYA ILIVYONOGA KWENYE VIWANYA VYA BOT CLUB

KAMPUNI ya bia ya TBL tawi la Mbeya imeahidi kuendeleza ushirikiano baina yake na wadau mbalimbali kwa kuhakikisha inatengeneza bidhaa zilizo na ubora na kukubalika na wateja. Ofisa matukio wa TBL kanda ya nyanda za juu kusini Francis Mwasamwene aliahidi hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya BOT Club jijini hapa. Mwasamwene alipongeza ushirikiano ambao umekuwa imara kwa kipindi kirefu baina ya kampuni na wadau hao hali inayowapa faraja kwa kuona wanakubalika na jamii inayowazunguka. Alisema kutokana na ushirikiano huo mzuri TBL imeendelea kujipatia mafanikio makubwa kupitia vinywaji inavyozalisha na kuviuza ndani na nye ya Tanzania. Alisema miongoni mwa mambo ambayo TBL kwa sasa inajivunia ni pamoja na kupata tuzo ya bia bora kupitia bia ya Safari aliyosema imezidi kupanua wigo wa soko la bidhaa zao. “Tuzo mbalimbali ambazo tumekuwa tukipata kupitia bia tunazozalisha ni matokeo ya ushirikiano mzuri baina yetu na wadau tunaofanya shughuli kwa karibu nao.Tuna imani ushirikiano huu utadumishwa.Na sisi kama TBL tunaamini kuzalisha bidhaa zinazokubalika ni chachu ya kudumisha ushirikiano huu” alisema. Aidha Mwasamwene alisema siku ya familia kwao ni chachu ya kuwawezesha wafanyakazi kukutana kwa pamoja na familia zao na kuweza kubadilishana mawazo na pia kufahamiana. Katika maadhimisho hayo wafanyakazi na familia zao walishiriki michezo mbalimbali ikiwemo kucheza muziki,kukimbiza kuu,kuvuta kamba na kukimbia kwenye magunia.

No comments:

Post a Comment