Friday, July 5, 2013
MRADI WA KUPINGA UNYANYASAJI WA KIJINSIA(GBV) WAZINDULIWA TUKUYU RUNGWE
Wafanyakari wa shirika na Watereeda na wa kikundi cha huduma
za majumbani(Kihumbe) Kushoto wakishindana kuvuta kamba na Watumishi
wa serikali wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwenye uzinduzi wa
Mradi wa majaribio wa kupinga Ukatili wa kijinsia(GBV) unaofadhiliwa
na mfuko wa rais wa arekani.Shindano lilimalizika kwa upande wa
Watereed na Kihumbe kushindaMkuu wa chuo cha Magereza cha Kiwira Kamishina Msaidizi
Mwandamizi Stanford Ntirundura akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya
soka ya Tukuyu Stars Afrika Ambele kombe baada ya timu hiyo kuifunga
Mpuguso Stars goli 4-2 katika mchezo uliochezwa kwenye uzindizi wa
mradi wa majaribio wa kupinga Ukatili wa kijinsia(GBV) unaofadhiliwa
na mfuko wa rais wa arekaniNahodha wa timu ya netiboli ya Tukuyu Queens Rehema Mwambusi
akionesha kombe kwa wachezaji wenzake(hawapo pichani) baada ya
kukabidhiwa na Mkuu wa chuo cha Magereza cha Kiwira Kamishina Msaidizi
Mwandamizi Stanford Ntirundura baada ya timu hiyo kuifunga goli 20-10
timu ya Magereza Queens kwenye uzindizi wa mradi wa majaribio wa
kupinga Ukatili wa kijinsia(GBV) unaofadhiliwa na mfuko wa rais wa
arekani.MMOJA WA WARATIBU WA GBV HIJJA WAZEE AKIUTAMBULISHA MRADI KWA WAKAZI WILAYANI RUNGWE KABLA YA MGENI RASMI KUUZINDUA
WACHEZAJI WA TIMU ZA NETIBOLI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA KUINGIA KATIKA MTANANGE WA KUMPATA BINGWA WA GBV KWA WANAWAKEBURUDANI YA IGIZO KUTOKA KWA WASANII WA KIKUNDI CHA KIHUMBE ILIKUWA KIVUTIO KINGINE KILICHOVUTA HISIA ZA WENGI WALIOHUDHURIA
KUTAKASWA kwa mwanamke aliyefiwa na mumewe kumetajwa kuwa sehemu ya
mila potofu zinazoendeleza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake
wilayani Rungwe.
Hayo yalibainishwa kwenye risala ya wakazi wa wilaya ya Rungwe kwenye
hafla ya uzinduzi wa mradi wa majaribio wa kupinga Unyanyasaji wa
kijinsia(GBV) iliyosomwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Tukuyu
Day Happy Joseph ambapo kwa wilayani hapa shirika la Watereed
litaendesha mradi huo kwa kushirikiana na Kikundi cha Huduma
Majumbani(Kihumbe).
Happy alisema licha ya serikali kwa kushirikiana na wadau wengine
kuendesha kampeni mbalimbali za kuelimisha jaamii juu ya kupinga
ukatili wa wa kijinsia bado jamii ya wanaRungwe imeendeleza mila ya
kuwatakasa wanawake kwa kuwalazimisha kufanya ngono na mwanandugu wa
mume kwa madai kuwa ni kumuondolea mwanamke husika mkosi alioachiwa na
mume aliyefariki.
Alisema tendo hilo limekuwa likiwakwaza sana wanawake kwakuwa licha ya
kutopewa nafasi ya kuchagua pia afya zao huwa hatarini kwakuwa ndugu
wanaolazimishwa kufanya nao ngono hakuna anayejua afya zao na wengine
huwa na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo virusi vya
ukimwi(VVU).
Alisema kupitia mradi wa GBV unaofadhiriwa na mfuko wa raisi wa
Marekani,wanawake wanaamini ni wakati sasa wa kuondokana na
unyanyasaji huo na kuomba waratibu wa mradi huo kujikita zaidi maeneo
ya vijijini kulikokithiri kwa unyanyasaji huo.
Kupitia risala hiyo pia wakazi wilayani hapa waliahidi kutoa
ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote cha miezi 18 ya mradi
kwakuwa ukatili ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wanawake na watoto ni
mkubwa na kwamba sasa hauvumiliki.
Akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela,mkuu wa chuo cha
Magereza cha Kiwira Kamishina Msaidizi Mwandamizi Stanford Ntirundura
alisema kaulimbiu GBV ya Amka sasa,Pinga ukatili wa
kijinsia,Mabadiliko yanaanza na wewe umekuja sehemu muafaka kutokana
na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto wilayani
hapa.
Ntirundura alisema wilaya hiyo pia bado inakabiliwa na mila za mume
kuwa na sauti katika umiliki wa mali zote na ndiyo sababu wanawake na
watoto wamebaki kuwa wazalishaji wakubwa wa mazao lakini hawanufaiki
na jasho lao kwakuwa mwisho wa siku mume huchukua fedha zote
zilizopatikana kutokana na mazao hayo na yeyeye kutumia ajuavyo.
Alisema ni wakati kwa wanaRungwe kubadilika kwa kuhakikisha wanatoa
taarifa kwa vyombo husika juu ya matukio ya unyanyasaji yanyofanywa na
wachache wanaoamini katika mila zisizoendana na wakati kwakuwa ni
kandamizi au zinahatarisha maisha ya watu wa kundi jingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment