Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, July 18, 2013

NJIWA MWENYE HIRIZI APELEKA BARUA LA ONYO KALI TAZARA

NJIWA aliyevishwa shanga na hirizi shingoni mwake huku akiwa amebeba ujumbe wenye onyo kali leo amesababisha taharuki kubwa katika ofisi za Shirika la reli kati ya Tanzania na Zambia(TAZARA) zilizopo jijini Mbeya. Ni baada ya kugundulika kuwa njiwa huo alikuwa ametua katika moja ya vyoo vilivyopo kwenye ofisi hizo ndipo wafanyakazi walijikuta kwenye wakati mgumu na baadhi yao kulazimika kuzikimbia ofisi zao. Majira ya saa mbili asubuhi ndipo mmoja wa watumishi wa Tazara alipobaini uwepo wa njiwa huyo na hapo ndipo mjadala mkubwa ukaibuka na kuvuta hisia za watu wengi wakiwemo wakazi wa maeneo ya jirani na ofisi hizo walioamua kufika kujionea. Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walikuwa ni miongoni mwa mashuhudawaliomuona njiwa huyo wa rangi nyeusi akiwa akiwa nyuma ya choo cha kiume kilichopo jirani na ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi shingoni iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni Nyekundu, Njano na Nyeupe. Hoja nzito ilihusu ujumbe uliokuwa kwenye barua aliyowasilisha njiwa huyo mahali hapo ambapo baadhi ya watumishi walionesha kumhisi mtumishi mmoja aliyetimuliwa kazi hivi karibuni kwenye mamlaka hiyo kutokana na ubadhirifu. Barua hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha mbili za Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili yalisomeka “ Naomba majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini” huku ikitaja orodha ya majina ya viongozi watatu wa wa shirika hilo. Ujumbe huo ulioonekana kuandikwa kwa mkono na kukolezwa kwa wino mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na maandishi yakiwa ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo. Mwajiri wa shorika hilo kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha kwa jina la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni wahudumu wa usafi. Mgweno aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu na wafanyakazi wenzake ambao walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho.

No comments:

Post a Comment