Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(Kushoto) na Mbunge wa Mbarali Dickson Kilufi wakisaini vitabu vya wageni baada ya kuwasili Ubaruku kuwasikiliza wananchi juu ya mgogoro wa mpaka kati ya vijiji 21 na Tanapa.
Moja ya mabango yaliyoandikwa ujumbe na wananchi wahanga wa uhamisho
Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu wakiwa na
Mwenyekiti wa CCM wilaya Mathayo Mwangomo baada ya kuhutubia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Mathayo Mwangomo baada ya kuhutubia wananchi.
HABARI KAMILI
KATIKA kuonesha hali si shwari ndani ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM) wilayani Mbarali,mbunge wa jimbo hilo Mbarali Dickson Kilufi na Mwenyekiti
wa CCM wilaya Mathayo Mwangomo,hivi karibuni nusura wapigane Mbelea ya waziri wa
Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
Nyalandu aliwasili wilayani humo majira ya jioni
kwajili ya kufuatilia mgogoro wa kimpaka wa ardhi kati ya Tanapa na wakazi wa vijiji
vilivyopo jirani na hifadhi ya taifa ya Ruaha katika eneo la Ihefu.
Baada ya kufika wilayani hapa ilikiwa Nyalandu
akutane kwanza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya wilaya ya Chama Cha Mapinduzi ili
kupata maoni yao kabla ya kukutana na uongozi wa serikali wilaya na kisha
wananchi katika kata ya Ubaruku.
Lakini kutokana na waziri kufika kwa kuchelewa
alilazimika kushauriana na viongozi wa chama kuahirisha vikao hivyo na badala
yake vifanyike kesho yake ili kutoa fursa kwa makundi yote kushirika katika
utatuzi wa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka saba sasa.
Hata hivyo mbele ya kiongozi huyo,Mbunge Kirufi na
mwenyekiti wake wa Chama walishindwa kuficha utofauti walionao na badala yake
walianza kurushiana maneno makali(matusi) mbele yake huku kila mmoja akionesha
kuwa mbabe zaidi ya mwenzie.
Chanzo cha habari cha uhakika kilichokuwepo eneo la
tukio kilieleza kuwa viongozi hao waliendelea kurushiana matusi hadi pale
Nyalandu alipoamua kuingilia kati kuwasuluhisha na baadaye yeye kuamua kwenda
jijini Mbeya kupumzika kabla ya kurejea wilayani hapa kesho yake.
Uthibitisho wa tukio hilo ulibainika katika ukumbi
wa CCM wilaya,wakati Nyarando alipowataka wawili hao wapeane mkono kuashiria
hali ya jana yake imekwisha mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya huku
pia akiwasisitiza viongozi hao kuwa na umoja katika kupigania maslahi ya chama
na wananchi wanaowaongoza.
Hata hivyo Mbunge Kilufi katika kuonesha kuwa bifu
halijakwisha licha ya kukubali kupeana mikono ukumbini,alipopanda jukwaani
mbele ya wananchi wa kata ya Ubaruku alionesha kuendelea kuwa na kinyongo mbelea
ya baadhi ya viongozi wa CCM wilaya japok hakuwataja majina.
“Hata kama unamchukia Kilufi,endelea
kumchukia,lakini katika suala la mpaka kati ya Tanapa na wananchi naomba
tuungane kuwatetea watu wetu” yalikuwa maneno ya Kilufi jukwaani.
Baadhi ya wakazi wilayani hapa wanasema ugomvi baina
ya wawili hao unatokana na kuwa ufuasi katika makundi mawili tofauti ya watu
wanaowania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao ambao mbunge anatajwa kuwa
katika kundi la waziri wa zamani Edward Lowasa.
Lakini wapo pia wanaosema mwenyekiti wa chama wilaya
amekuwa akipingana na mbunge huyo katika suala la mpaka kati ya Tanapa na
vijiji vya jirani kwa kile wanachoeleza kuwa amekula rushwa kutoka Tanapa
tuhuma alizozitaja pia mwenyekiti huyo alipozungumzia suala la mpaka akiwa
ukumbini.
“Mh.waziri suala hili la mpaka wengine hata
limetupaka matope,wapo wanaosema tumeingizwa mifukoni mwa Tanapa.Wanasema
Tanapa wametununua kwa kutupa fedha ili tusiwatetee wananchi.Tunaomba tulipatie
ufumbuzi ili mambo haya yasiendelee” alisema Mwangomo alipokuwa ukumbini.
No comments:
Post a Comment