Hawa ndiyo waliobinafsishiwa kiwanda na sasa hakifanyi kazi.Majengo yamegeuka mradi wa maghala kupangishia kampuni nyingine.
KILIO kikubwa kwa
vijana wa kitanzania ni ukosefu wa ajira kwa kundi hilo muhimu.Moja ya mambo
yanayokwamisha upatikanaji wa ajira katika maeneo mbalimbali ni pamoja na sera
mbovu ya ubinafsishaji wa makampuni na
viwanda vya umma uliofanyika miaka kadhaa iliyopita.
Ubinafsishaji huu ambao
haukuzingatia maslahi ya watanzania walio wengi,ulifanyika huku watawala
wakijua watu wanaobinafsishiwa hawana uwezo wa kuendesha Makampuni ama viwanda
wanavyobinafsishiwa.
Kiwanda cha Zana Za
Kilimo maarufu kama ZZK ni moja kati ya viwanda vilivyokuwa vikizalisha ajira
kwa wingi na kutoa ukombozi wa kiuchumi kwa vijana wa mkoa wa Mbeya na mikoa ya
jirani.Lakini kiwanda hiki kama ilivyo kwa vingine kilibinafsishwa kwa mtu asiye
na uwezo wa kukiendesha.
Hivi sasa mmiliki wa
kiwanda hiki ambacho mashine na vipuri vinaendelea kuozea ndani ya majengo huku
pia vikiwa vimegeuka makazi ya mijusi na nyoka wenye uwezo wa kuishi maeneo ya
baridi hakiendeshi.Badala yake amegeuka baba mwenye nyumba na kuanza kupangisha
majengo ya kiwanda hiki kwa makampuni mengine.
Moja kati ya kampuni
zilizopanga mahali hapa ni kampuni ya SBL ambayo inatumia sehemu ya majengo ya
kiwanda hiki kama maghala ya kuhifadhia bidhaa zake yaani bia.
Lakini wakati
watanzania hususani vijana wa mkoani Mbeya wakilalamikia kufungwa kwa kiwanda
hiki,vijana wachache wanaonekana wasaliti kiasi cha kufurahia hata uzinduzi wa
ghala hili kama unavyowaona kwenye picha mbalimbali za hapo juu wakicheza baada
ya kupewa bia za bureeeeee.
Viongozi nao walishiriki
kwenye uzinduzi wa ghala hili kama unavyowaona wachache kwenye hizo picha.Wapo
viongozi waliostuka na kukacha ufunguzi huo,lakini kwa kuogopa lawama za mabosi
wa kampuni hii wakawatuma wawakilishi.
Sote tujiulize,hivi
mwekezaji huyu alipewa kiwanda ili azalishe zana za kilimo au kupangisha
majengo kwa makampuni mengine.Na je kama vijana wa kitanzania hawawezi kuwa na
msimamo kiasi cha baadhi kufurahia wakati wengine wanalia ni lini kilio chao
kitasikilizwa?
No comments:
Post a Comment