Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, October 13, 2015

ZIARA YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA KIJIJINI LUTETE RUNGWE

 Mwanahabari mkongwe Jonas Mwasumbi akiwaelekeza wanahabari juu ya masuala ya kilimo cha mazao mbalimbali baada ya kuwapokea nyumbani kwake kijijini Lutete wilayani Rungwe.



Wanahabari wa mkoa wa Mbeya wakiongozwa na mwenyekiti wao Modestus Nkulu(aliyenyenyua mkungu wa ndizi) wakifurahia matunda kutoka katika shamba la mwenyeji wao.
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo akifurahia jambo kwenye gari wakiwa njiani kuelekea kijijini Lutete.



 Ziara ya kutembelea shamba ikiendelea 


Mwanahabari  Mwasumbi akiwaelekeza wanahabari juu ya masuala ya kilimo cha nanasi.



Mwanahabari na katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Emmanuel Lengwa akinywa maji ya asili ya kijijini Lutete.Wanahabari wengi walifurahia ladha nzuuri ya maji hayo.



Wakiwa wameruhusiwa na mwenyeji wao kuishi kama wapo nyumbani wanahabari walivamia matunda yaliyokuwa yameiva shambani.Hapa Derick Lwasye na Ally Kingo wakiangua matunda aina ya papai.
 Hakika wanahabari walifurahia utamu wa matunda kutoka katika bustani ya mwenyeji wao mzee Mwasumbi.Hapa mwanahabari Ally Kingo akiendelea kula matunda.
Baada ya kukamilisha ratiba ya siku ya kwanza wanahabari walijumuika na baadhi ya wenyeji wa kijiji cha Lutete kubadilishana mawazo wakati wakipata vinywaji moto na baridi.
TUTAENDELEA KUKULETEA MATUKIO ZAIDI...ENDELEA KUWA NASI............

3 comments:

  1. Mungu awatie nguvu ndugu jamaa na marafiki hasa tasnia ya habari kwa kuondokewa na baba yetu mpendwa Mzee Jonas Mwasumbi. Poleni sana wanahabari kwa pigo hili.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wote wana mbeya na watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wetu J Mwasumbi mungu AWATIYE nguvu kwa ktk kipindi hiki kigumu, bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete
  3. ooh my Gog!!! i new it today. mungu amlinde mahali peeema peponi na poleni ila tujitaidi tuwe kama yeye
    \

    ReplyDelete