TIMU ya Soka ya Viongozi
na watumishi wa Serikali mkoani Mbeya inatarajia kumenyana vikali na timu ya
Viongozi wa dini mkoani hapa,katika mchezo utakaopigwa ndani ya iwanja wa
Sokoine jijini Mbeya siku ya Mei mosi.
Mchezo huo utakaopigwa
jioni mara baada ya kumalizika kwa shughuli za Sherehe za Maadhimisho ya Siku
ya wafanyakazi duniani unatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa kutokana na watu
watakaoingia uwanjani hapo kuushuhudia wakianzia na matukio ya sherehe.
Akizungumzia mchezo
huo,mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ambaye pia ni Kocha mchezaji ndani ya
kikosi cha viongozi wa Serikali leo ametamba kuhakikisha wanaibuka na ushindi
mnono dhidi ya viongozi wa dini.
Amesema ushindi huo utakuwa
kulipiza kisasi kwani miaka kadhaa iliyopita,timu hizo ziliwahi kumenyana ndani
ya dimba la Sokoine na viongozi wa serikali wakaambulia kichapo.
Amewasihi wakazi mkoani
hapa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mpambano huo akisema itakuwa sehemu pia ya
wao kujifunza kuwa viongozi nao wako tayari kuonesha mfano wa ushirikiano bora kwa
vitendo.
Akizungumzia kambi ya
Viongozi wa dini,Meya wa jiji la Mbeya,Mchungaji David Mwashilindi amesema
kwakuwa yeye atacheza upande wa viongozi wa kidini ana uhakika historia
itaendelea kujirudia kwa viongozi wa Kiserikali kufungwa.
No comments:
Post a Comment