Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, April 30, 2017

MAAGIZO YA JPM AKIWA DODOMA

Kabla ya kuondoka Dodoma kwenda Kilimanjaro Mhe. Rais Magufuli ameagiza mambo manne.

1. Chuo Kikuu cha Dodoma kifutiwe deni la kodi ya ardhi la zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kama ilivyoombwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Prof. Kikula.


2. Hati za viwanja za Dodoma zilizokuwa zinatoa umiliki wa miaka 33 tu ziongezwe hadi kufikia miaka 99 ili kuvutia uwekezaji.


3. Uwanja wa mpira ambao Mfalme wa Morocco Mohammed VI ametoa msaada wa kuujenga Dodoma, ujengwe jirani na Mjini.


4. Wizara ya Ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na vyombo vingine vinavyohusika wakae na kufanya tathimini kama bado tunahitaji kuendelea kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).

No comments:

Post a Comment