Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, June 7, 2017

ZIARA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA SAUT KISIWANI SAANANE

Wanafunzi wa Sociology mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustin(SAUT) cha Mwanza wakiruka kwa furaha katika moja yam awe makubwa ambayo ni kivutio ndani ya hifadhi ya Saanane ndani ya Ziwa Victoria.
Hapa wanafunzi wakifurahia jambo wakiwa kwenye boti maalumu la kitalii.Katika hifadhi ya Kisiwa hiki chenye vivutio lukuki,Wanyama wakali kama Simba waliondolewa na kubakia Wanyama wapole kama Swala, Pundamilia na Ndege wa aina mbalimbali.


Mmoja wa wanafunzi hao Lummie Julius Tupa akiwa katika pozi kwenye moja ya maeneo ya mapumziko kisiwani hapo
 Michezo mbalimbali iliendelea Kisiwani hapa,hakika ilikuwa siku ya kipekee na isiyosahaulika,ukiwa Hifadhini saanane hautoishia kuona wanyama kama Swala, Pundamilia na Ndege pekee yapo mambo mengine meengi ya kuvutia.


No comments:

Post a Comment