Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, October 7, 2012

HATARINI KUPATA KIPINDUPINDU

WAKAZI wa kata ya Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa wapo hatarini
kupata magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu kutokana na kuendelea
kutumia maji yasiyo safi wala salama.

Hali hiyo inatokana na uhaba mkubwa wa maji unaovikabili vijiji vya

kata hiyo ambapo sasa wanalazimika kunywa maji yanayochotwa kwenye
madimbwi yanayotumiwa pia na mifugo ikiwemo ng’ombe.

Hatari zaidi ni pale ambapo tayari vijiji kadhaa vilivyopo jirani na

kata hiyo kemeripuka ugonjwa wa kipindupindu na tayari hatua kadhaa
zinachukuliwa na serikali ya wilaya kuhakikisha ugonjwa huo hauenei
kwenye maeneo mengine.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtenga Angelina Ndotela alisema

wanalazimika kutembea umbali mrefu wa takribani kilometa tatu kufuata
maji kwenye madimbwi yaliyopo kwenye mbuga ambapo pia ndiko wafugaji
hunywesha maji mifugo yao.

“Kwa sasa tunaishi kwa kudra za mwenyezi mungu.Maana maji tunayotumia

kwakweli kikizuka kipindupindu hapa kama tunavyosikia kwenye vijiji
vya jirani sijui kama tutapona.”alisema Ndotela.

Alisema hali hiyo imegeuka neema kwa baadhi ya wakazi hususani vijana

ambao wamekuwa wakitumia pikipiki na baiskeli kuyafuata maji hayo na
kasha kuwauzia wakazi wenzao kwa shilingi 500 kila lita 20.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Alexanda Kapele

alikiri kijiji kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali inayolazimu
wakazi kutembea umbali mrefu kuyafuata maji yasoyo safi wala salama
kwa matumizi ya binadamu.

Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Mtenga anayekaimu pia nafasi ya

afisa mtendaji wa kata Daniel Kalumbilo alisema uhaba wa maji katika
vijiji vya kata hiyo unatokana na ukame uliopo uliosababishwa na ujio
wa wafugaji wa kabila la kisukuma ambao wamepeleka idadi kubwa ya
mifugo kupita uwezo wa eneo lililop

No comments:

Post a Comment