Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, October 9, 2012

UWINDAJI PANYA CHANZO CHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA


UWINDAJI wa panya (Kacheko kwa lugha ya Kifipa) na wanyama wengine wadogo wadogo kwaajili ya kitoeo umetajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayochangia kuchomwa kwa misitu katika kata ya Sintali wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Mmmoja wa wakazi wa kata hiyo Sabasi Severino Mafua ameeleza hayo alipokuwa akichangia mada kwenye mdahalo wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika katika kata hiyo jimbo la Nkasi kusini ulioandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani hapa (Nkangonet) ukiwa umedhaminiwa na shirika la The Foundation For Civil Society.

Mafua amesema kwa sehemu kubwa kuchomwa kwa mapori kunakofanyika kwenye vijiji vya kata hiyo kunatokana na wakazi kutafuta kitoeo aina ya panya na wanyama wengine wadogo ambao unapochoma msitu ndipo urahisi wa kuwakamata ama kujua wanakojificha unakuwepo.

“Wengi wanachoma ili wapate kitoeo aina ya panya maana ni desturi ya wakazi wa kata hii na wafipa kwa ujumla kula panya kama kitoeo.Na hata ukienda vilabuni utakuta wamechomwa na wanauzwa kwa bei tofauti tofauti.Sasa wachimbaji wa panya hao hulazimika kuchoma mapori ili iwe rahisi kuwakamata.Vivyo hivyo na tuwanyama twingine tudogo tunatopatikana kwenye mapori na vichaka kama panya” anasema.

No comments:

Post a Comment