JESHI la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu
wawili wakikabiliwa na tuhuma za kusambaza Ujumbe wenye kuashiria kuhatarisha
amani ya nchi kupitia mtandao wa simu hatua inayohusishwa na Tukio la Oparesheni Ukuta lililopangwa na
Chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) lifanyike Septemba mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri
Kidavashari,wanaoshikiliwa ni pamoja na mkazi wa kata ya Isanga jijini Mbeya Moses
Mwaifunga(28) na Meshaki Mgaya(28)mkazi wa Ileje mkoani Songwe.
Kadhalika kamanda Kidavashari amesema leo kuwa jeshi hilo
linawatafuta watuhumiwa wengine Emma Kimambo na Moris Chanonga ambao amesema
popote walipo wanapaswa kujisalimisha wenye katika vituo vya polisi vilivyopo
jirani nao.
Anasema watuhumiwa hao wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa
Chadema,wamehusika kusambaza jumbe mbalimbali unaoashiria kutokubaliana na
agizo la serikali la kukataza kufanyika kwa uparesheni Ukuta kwakuwa Jumbe
wanazosambaza zinashinikiza wafuasi wa chama hicho kutokata tama bali
wajitokeze kushiriki oparesheni hiyo.
Anasema zipo baadhi ya jumbe ambazo watu hao
wameonesha nia ya kufanya Oparesheni Ukuta hata kabla ya kuwadia kwa siku
iliyokuwa ikitajwa na Chadema yaani Septemba Mosi huku pia nyingine zikionesha
wamedhamiria kufanya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuchoma ofisi za Chama
Cha Mapinduzi(CCM).
Kamanda Kidavashari anaonya wafuasi wa Chadema na
wananchi wengine kuepuka kusambaza jumbe zinazoonekana kukiuka miiko na maadili
ya Utaifa na pale wanapotumiwa kabla ya kuzituma kwa watu wengine wazifute au
kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.
Amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa
na mamlaka huku akisisitiza kuwa hata maandiko matakatifu katika baadhi ya
vitabu vya dini yanaeleza kuwa Kila Mamlaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment