Mwanahabari Fredy Jackson akichangia maoni katika warsha ya
mafunzo ya uandishi wa habari za Ukimwi na Ukatili wa kijinsia na wa watoto
iliyofanyika mkoani Mbeya
Wanahabari wakipitia nakala ya gazeti la habarileo kuona
iwapo lina japo habari moja inayohusu ugongwa wa Ukimwi walipokuwa kwenye
makundi kwenye wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya uandishi wa habari za
Ukimwi,ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto yaliyoandaliwa na ofisi
ya mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mbeya kwa ufadhili wa shirika la kuhudumia watoto
duniani(Unicef).
Mwanahabari mkongwe Charles Kayoka akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za Ukimwi na
ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto
HABARI KAMILI
KUENDELEA kwa mfumo dume katika jamii kumeonekana
kuzidi kuendeleza ukatili dhidi ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kutokana na
mama zao kuficha ukweli kwa kutowaeleza waume zao kuwa si baba wa watoto hao.
Kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 1971 ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,miongoni mwa haki alizonazo mtoto ni pamoja na
kuwafahamu wazazi wote wawili na ndugu zao.
Lakini katika jamii baadhi ya watoto wameendelea
kufichwa baba zao halisi kutokana na wanawake kutokuwa na nguvu ya kubainisha
ukweli juu ya watoto hao kwa waume wanaoishi nao tofauti na ilivyo kwa wanaume
wanaozaa nje ya ndoa.
Hali hiyo ilibainika pale wanahabari mkoani Mbeya waliopo
kwenye mafunzo ya Uandishi wa habari za VVU/Ukimwi na Ukatili wa kijinsia na
ukatili dhidi ya watoto walipozungumza na baadhi ya wakazi katika mji wa
Mbalizi wilayani Mbeya.
Wakizungumza katika maeneo tofauti mjini hapo baadhi
ya wakazi hao walisema wanawake wanaozaa watoto wao nje ya ndoa zao hawana
uwezo wa kuwatambulisha watoto hao kutokana na hofu ya kuvunja ndoa zao pale
inapobainika tofauti na ilivyo kwa wanaume.
Baadhi ya wakazi Joyce Mwile,Vanesa Muhada na Shayo
Katina walisema kutokana na mfumo dume habari zimekuwa zikizagaa katika jamii
juu ya uwepo wa wanawake walio ndani ya ndoa kuzaa nje ya ndoa zao lakini
wanawake hao hawaweki wazi masuala hayo kwa waume zao.
“Wanaume wanaweza na wamekuwa wakifanya hivyo mara
nyingi.Hii inatokana na mfumo wa kimaisha tangu kuumbwa kwa dunia hii.Na kama
ni haki ya mtoto kuwajua wazazi basi wapo watoto wengi wanaofanyiwa aina hii ya
ukatili” alisema Katina.
Hali hii inaonekana kuwa mbaya zaidi pale ambapo
viongozi wa dini nao wanashauri kuendelea kutunzwa kwa siri juu ya watoto
wanaotokana na mimba zilizotungwa nje ya ndoa kwa madai kuwa kufanya hivyo
kutawezesha ndoa kutovunjika.
Mchungaji Erick Kombe wa kanisa la Consuming Fire
Centre tawi la Nsalala Mbalizi alisema kuna uwezekano pia wa wanawake kuuawa
iwapo watatoa siri kwa waume zao iwapo walichepuka na kuzaa nje ya ndoa
Wajibu wa jamii katika kuwezesha watoto wanaozaliwa
nje ya ndoa ni kutafuta namna itakavyowawezesha wanawake nao kuanza kuweka
bayana juu ya mimba zinazotungwa nje ya ndoa kama ilivyo kwa wanaume lengo
likiwa ni kuwapa watoto haki ya msingi ya kuwatambua wazazi wao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment