Wanafunzi kutoka shule mbalimbali
mjini Tunduma Momba wakiwa barabarani kuandamana kwa kutaka serikali kujenga
matuta katika barabara ya Mbeya Sumbawanga kutokana na mwanafunzi mwenzao
kugongwa na kufa pamoja na wengine kujeruhiwa huku Polisi wakijaribu kuangalia hali ya usalama
Mkuua wa wilaya ya Momba Abiud Saidea akiwasili eneo la tukio
HABARI KAMILI
WANAFUNZI wa shule Mbalimbali
za msingi wilayani katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba Mkoani
Mbeya,wameandamana barabarani wakiishinikiza Serikali kujenga matuta
katika barabara inayo toka Mjini Tunduma hadi Sumbawanga mkoani
Rukwa kutoka na kutokea kwa ajari za mara kwa mara.
Maandamano ya wanafunzi hao hayo
yametokea leo asubuhi majira ya saa 3 ni baada ya Wanafuzi wawili
kugongwa papo hapo na kusababisha mmoja kuaga dunia na wawili kuwa majeruhi
katika ajari iliyo tokea jana katika maeneo ya Transforma mtaa wa Mwaka
wilayani hapa.
Wakizungumza maeneo ya
mandamano katika umati wa wanafunzi wa shule hizo, huku wakiimba
nyimbo za kuishinikiza serikali kujenga matuta eneo hilo ambalo
limekuwa likisababisha ajari mara kadhaa.
Wasema eneo la Transifoma
ni eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likisababisha ajari kutokana na
kukosekana kwa matuta ya kuzuia mwendokasi wa magari bila kujali
kuwa ni kivuko cha wanafunzi.
“Tunaitaka serikali kutujengea
matuta eneo hili maana wanafunzi wengi wamepoteza maisha kwa kugongwa na magari
” alisema mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Ally.
Hata hivyo waliishinikiza
seikali kwa kuitaka iharakishe kuchukua hatua hiyo mara moja ili kuepusha
majanga hayo.
Pia,kwa upande wa Wananchi
wamesema kuwa ni haki yao kwa wanafunzi hao kudai haki yao na ukiangalia idadi
ya watu waliogongwa na magari katika eneo hili ni Wakubwa ni watu nane na
watoto 10 kitu ambacho kinasadikika ni mwendokasi wa Madereva.
Akizungumza mbele ya umati wa
wanafunzi diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka aliitaka serikali
kuanza mara moja ujenzi wa matuta hayo ili kupunguza ajari za wanafunzi na watu
wazima maeneo hayo.
“Tunaitaka serikali kuanza leo
ujenzi wa matuta eneo la Transfoma maana tumechoka kupoteza maisha ya watu kwa
ajari zinazo zuilika” amesema Mwakajoka.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Momba Abiudi Saidea amewata wanafunzi pamoja na wazazi kuwa watulivu wakati
serikali ikitekeleza ujenzi wa matuta eneo hilo hatari , lililopoteza maisha ya
watu wengi.
Amesema ujenzi huo utaanza
mara moja bila kuchelewa , na aliwahidi kuwa ameshaongea na uongozi wa Tanroad
wa makao makuu ya mkoa wa Mbeya ili waje wapime eneo hilo na kuanza
ujenzi wa matuta hayo.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII
No comments:
Post a Comment