Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akisalimiana na mbunge wa Ileje Aliko Kibona wakati waziri huyo alipowasili wilayani Ileje kukagua barabara ya Mpemba Isongole inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.Wengine ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Mohamed Mwala(kushoto) na mkuu wa wilaya Rosemary Senyamule.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akikagua daraja
la mto Songwe linalounganisha nchi ya Tanzania na Malawi kupitia mpaka wa
Isongole wilayani Ileje alipokuwa ziarani wilayani hapo.Kushoto kwake ni mkuu
wa wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akishirikiana na
maafisa kutoka wizara yake na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Ileje kukata
utepe kuzindua barabara ya Isongole-Itumba iliyojengwa na serikali kwa kiwango
cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akipongezana na mbunge wa Ileje Aliko Kibona baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa barabara ya Isongole-Itumba iliyojengwa na serikali kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akizungumza na
wakazi wa mji wa Isongole wilayani Ileje alipokuwa katika ziara yake mkoani
Mbeya.Akiwa Ileje Dkt Magufuli aliwahakikishia wakazi hao kujengwa kwa kiwango
cha lami barabara ya Mpemba-Isongole na kubainisha kuwa serikali inaendelea
kufanya mazungumzo na serikali ya Malawi ili kuona uwezekano pia wa barabara
kutoka mpaka wa Isongole inajengwa kwa kiwango hicho upande wa Malawi.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akifurahia zawadi
ya Mwiko na jamvi la asili aliyokabidhiwa na kikundi cha wanawake wajane wa
wilayani Ileje.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akihutubia mamia
ya wananchi wakazi wa Rujewa wilayani Mbarali katika mkutano uliofanyika mjini
hapo,ajenda kubwa ikiwa ni ujenzi wa kipande chaa barabara kutoka Igawa hadi
Ubaruku kinachoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami ambapo serikali
imesisitiza kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ili kuwezesha mpunga
unaozalishwa kusafirishwa.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akishirikiana
na mbunge wa Mbarali Dickson Kilufi kukata utepe kuzindua barabara ya
Igawa-Ubaruku wilayani Mbarali inayoendelea kujengwa kwa awamu kwa kiwango cha
lami
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo akiwa pembezoni mwa daraja la Mto Songwe linalotenganisha nchi za Tanzania na Malawi kupitia mpaka wa Isongole wilayani Ileje.
Mbunge wa Ileje Aliko Kibona akicheza ngoma ya asili iliyopigwa na moja ya vikundi vya sanaa wilayani IlejeMkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha waziri wa Ujenzi kuhutubia wananchi.
Watoto wataalamu wa mashairi ya kujigamba wakionesha kazi yao mbele ya waziri alipokuwa wilayani Ileje.
Dkt.Magufuli akisalimiana na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali mara baada ya kuwasili wilayani hapo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Hussein Kandoro akizungumza jambo mbele ya wakazi wilayani Mbarali kabla ya kumkaribisha waziri kuhutubia.
No comments:
Post a Comment