Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 6, 2015

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA,SHERIA NA UTAWALA YATEMBELEA MIRADI YA TASAF MBARALI

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoroakifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga.
 MKuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhussein Kifu(wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabla ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na UtawalaVedastus Rweyikiza akizungumza jambo baada ya kamati hiyo kukutana na wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya.

Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza kabla ya kuanza kugawiwa fedha kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo jana.
 

 Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani Hellena Bamba akikabidhiwa fedha kutoka kwa kamati ya mradi ya wilaya(CMC).

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wakiangalia namna wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani wanavyokabidhiwa fedha.Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza kushoto kwake akifuatiwa na Felix Mkosamali na Willium Ngeleja.



 Mmoja wa wanufaika wa mpango akielezea manufaa aliyoyapata baada ya kuanza kuhamilishiwa fedha.
Wajumbe wa kamati ya bunge wakiwaaga wanufaika wa mpango katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarali mmkoani Mbeya. 
  

                            HABARI KAMILI

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Wajumbe wameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa mpango huo,baada ya jana kukutana na walengwa na kufanya mahojiano nao ambapo wengi wa wa wanufaika walibainisha namna ambavyo fedha walizohawilishiwa zimewaletea mabadiliko kimaendeleo.

Katika maelezo yao mbele ya wajumbe wa kamati ya bunge, baadhi ya walengwa wameeleza namna walivyonufaika na fedha zilizokwishatolewa ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto,kuboresha makazi yao na kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya na lishe.

Baadhi ya wanufaika Hellena Bamba,Amina January na Spedito Kinyaga wamesema mpango wa kunusuru kaya masikini umewawezesha pia kuanza kumudu maisha yao kwani wameweza pia kupata elimu ya kujikomboa kiuchumi kwa kujihusisha na shughuli kama za ufugaji kuku na kilimo cha kisasa japo kwa mashamba madogo madogo.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini Madabaga,mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza amewahimiza wananchi hao kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ikiwa ni pamoja na kubuni miradi itakayowafanya wawe katika mazingira mazuri hata baada ya mpango huo kumalizika.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Ladslaus Mananga,mkurugenzi wa ukaguzi wa mfuko huo,Christopher Sanga alibainisha kuwa jitihada za kuwafikia walengwa wote wa mpango huo zinaendelea ambapo ifikapo katikati ya mwaka huu zaidi ya kaya milioni moja zitanufaika na utaratibu wa uhawilishaji fedha nchini kote.



No comments:

Post a Comment