Waziri
wa chi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk.Binilith Mahenge akiwasikiliza raia wa China ambao ni viongozi wa Kiwanda cha Sunshin Mining ambao muda mwingi raia hao wawili ambao haikufahamika nani ni bosi kwa mwenzake walitumia zaidi lugha ya kichina kuliko kingereza kila walipoulizwa jambo.
Waziri
wa chi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk.Binilith Mahenge akionesha namna
miti iliyopo ndani ya bwawa ilivyokauka kutokana na sumu iliyopo kwenye maji
yanayotoka kiwandani.
Sehemu
ya msitu wa asili ambao miti yake imekauka kutokana sumu ya maji kutoka kiwanda
cha kampuni ya Sunshine Mining
Sehemu
ya msitu wa asili ambao miti yake imestawi kutokana na kutokuwa ndani ya bwawa
la maji yenye sumu
Wanahabari
wakipiga picha bomba linalotiririsha maji kutoka kiwanda cha unhenjuaji dhahabu
kinachomilikiwa na kampuni ya Sunshin Mining
Eneo zinakoishia taka za vyoo likiwa limejengwa kiholela huku pia likifunikwa juu kinyume na utaratibu wa utunzaji wamzingi katika maeneo ya migodi na viwanda unavyoelekeza.
HABARI KAMILI
SERIKALI imetishia kukifungia kiwanda cha uchenjuaji
dhahabu kinachomili kiwa na kampuni ya Sunshine Mining kilichopo wilayani
Chunya iwapo uongozi wa kampuni hautafanyia kazi mapungufu yaliyopo kiwandani
hapo.
Waziri wa chi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
Dk.Binilith Mahenge alitoa muda huo wa marekebisho alipotembelea na kujionea
mapungufu kadhaa yaliyopo ikiwa ni pamoja na kiwanda kutoajiri afisa mazingira.
Mapungufu mengine yaliyopo ni kampuni kutojenga
bwawa kwaajili ya kuhifadhia maji machafu yanayotoka kiwandani yakiwa
yanaambatana na kemikali aina ya Sodium Cyanide ambayo inaathari kubwa katika
afya ya viumbe hai ikiwemo binadamu.
Badala yake kampuni hiyo imejenga ukuta mnne wa
kifusi na kuzuia moja ya mabonde ambayo ni chanzo cha maji yam to Lupa na
kutumia sehemu ya bonde hilo kuwa bwawa la kuhifadhia maji machafu hali
iliyosababisha pia viumbe hai ikiwemo miti kukauka kufuatia kemikali na kwakuwa
bwawa hilo halijsakafiwa chini.
Kasoro hizo ndizo pia zilisababisha Julai mwaka jana
maafisa wa Barza la Usimamizi wa mazingira nchini(NEMC) kukifungia kiwanda
hicho lakini baada tu ya maofisa hao kuondoka uongozi ulikiuka na kuendelea na
shughuli za uzalishaji kama kawaida.
No comments:
Post a Comment