JESHI
la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi askari wake wawili kutokana na askari
hao kuwafanyia Vitendo vinavyokwenda kinyume cha maadili wanafunzi wa kike wa
kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na
Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Dhahiri
Kidavashari amewataja askari waliofukuzwa kazi kuwa ni H.4925 PC Petro Oscar
Magana wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na J.1422 PC Lucas Joseph Ng’weina
wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.
Kamanda
Kidavashali amesema leo kuwa mnamo Novemba 4 mwaka huu majira ya saa 5:30 Usiku huko
katika Shule ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya
Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari hao wawili wawili wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na
maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa Shule hiyo wanaoendelea na
mtihani wa Taifa.
Amesema
kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya
kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa kile
walichodai kupiga kelele.
Amesema
baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa
adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na
kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali
na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoka na kurudi majumbani kwao”.
Amesema
Kufuatia vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo,Rose Dihembe alitoa taarifa kwa
uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa Mkoa ambao mara moja
walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali ikiwemo kusikiliza
malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari waliolalamikiwa na mwisho
kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea kufukuzwa kazi askari hao.
Hata
hivyo kamanda Kidavashari amesema kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao
jeshi la polisi linatarajia kuwafikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi
kukamilika.
Kamanda
huyo, ametoa wito kwa wananchi mkoani hapa kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi na
kwamba halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili
ya kazi yao na pia kinyume na sheria za nchi.
Aidha
Kamanda Kidavashari ameomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vyote
vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au wananchi wa
kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment