Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Mkalla (kulia) akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama mkoa na viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu mkoani Mbeya wakikagua Miundombinu ya Uwanja wa Ndegea wa Kimataifa wa Songwe(SIA).Lengo la ziara hii iliyofanyika jana ni kuwezesha wananchi kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Usafiri nchini
Mkuu wa Usalama katika uwanja wa SIA Ole Laput akitoaa maelekezo juu ya masuala ya usalam uwanjani SIA
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Mkalla akifafanua jambo kwa wajumbe alioongozanaa nao kwenye ziara ya kukagua uwanja wa SIA
Mhariri Mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw. Joachim Nyambo akikagua taa za kuongozea ndege wakati wa mchana kunapokuwa na ukungu. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Mkalla na wajumbe wengine wakisikiliza maelezo ya Uongozaji ndege kutoka kwa mhandisi Samweli Murembe aliyekuwa zamu kwenye Chumba cha kuongozea ndege Juu ni Viongozi wa dini na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mbeya wakiangalia namna tukio la uzimaji moto linavyofanyika iwapo kutatokea ajali ya ndege kuwaka moto ikiwa uwanjani.Chini ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Mkalla akishirikiana na viongozi wa dini kuuombea uwanja wa SIA
HABARI KAMILI
WAKAZI mkoani Mbeya wamehamasishwa kujiandaa na ujio
wa Ndege za Kampuni ya ATC zinazotarajiwa kuanza safari za Dar es salaam na
Mbeya kuanzia DDesemba 2 mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa hamasa
hiyo alipofanya ziara na viongozi wa dini mkoani hapa kutembelea Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Songwe(SIA) lengo likiwa ni kujinea jitihada zinazofanywa
na Serikali za kuukamilisha uwanja huo.
Makalla amesema taarifa zilizothibitishwa kuwa ndege
za ATC zitakuwa zikifanya safari kwa siku tano kwa juma ambapo siku hizo ni
Jumatatu,jumatano,ijumaa,jumamosi na jumapili.
Amesema ndege ndege itakuwa ikitoka Dar es salaam
saa sita mchana na kufika Mbeya saa nane na kisha saa nane na nusu kuanza
safari ya kurudi Dar es salaam.
Amesema kutokana na fursa hiyo wakazi wa mkoa wa
Mbeya na maeneo ya jirani wanapaswa kujipanga kuhakikisha wanakuwa wanufaika wa
kwanza kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazoweza kuzifanya kupitia
fursa hiyo
Aidha mkuu huyo wa mkoa pia amesisitiza adhma ya
mkoa wa Mbeya kunufaika na uwanja wa SIA kwa wawekezaji kuzalisha na
kusafirisha maua,matunda na mbogamboga kwenda nje ya nchi mara ndege za
kimataifa zitakapoanza kutua kwenye uwanja huo.
Amewataja
viongozi wa dini kuwa moja ya kundi muhimu linaloweza kuwahamasisha
wananchi kuutumia uwanja huo kwa manufaa huku akiwasisitiza pia kutumia nafasi
walizonazo kuhubiri amani ili uwanja huo uweze kuwa katika hali ya usalama
wakati wote.
Kwa upande wao viongozi wa Dini walioshiriki ziara
hiyo,wameipongeza serikali kwa jitihada zake za ujenzi wa uwanja wa SIA
hususani hatua ya kufunga Taa za kuongozea ndege wakati wa Ukungu wakisema
zitasaidia kwa kiasi kikubwa safari za ndege kuwa za uhakika.
Wameisihi serikali kuendelea kushughulikia
changamoto ya kufunga taa za kuongozea ndege wakati wa usiku ili kuwezesha
ndege kuanza kufanya safari zake wakati wote wakisema itawezesha uwanja huo
kutumika kwa tija zaidi.
No comments:
Post a Comment