WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya katika
matukio tofauti yakiwemo mawili ya mauaji ya kinyama.
Miongoni mwa matukio ya mauaji hayo ni pamoja na la mkazi
wa kijiji cha Mkutano wilayani Momba,Hamis Simwawa(25) aliyekutwa shambani
akiwa ameuawa kwa kukatwa shoka shingoni na kisha kunyofolewa viungo vya mwili
ikiwemo ulimi,meno ya chini na jicho la kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki
mwili wa Hamis ulikutwa Januari 26 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi katika
kijiji cha Mkutano kilichopo katika kata
ya Nzoka wilayani Momba.
Kaimu kamanda Masaki alisema kabla ya mauaji kijana
huyo aliitwa kwenda kusaidia shughuli za shamba na alipofika shambani ndipo walimuua
kwa kumkata na shoka shingoni kabla ya kumnyofoa ulimi,meno ya chini na jicho
la kushoto na kupeleka viungo hivyo kusikojulikana.
Alisema tukio hilo linahusishwa na imani za
kishirikina na kufuatia mauaji hayo watu wawili wanashikiliwa aliowataja kuwa
ni Kawawa Sinkala(31) na Emmanuel Sinkala(15) wote wakazi wa kijiji cha
Mkutano.
Katika tukio la pili Kaimu kamanda Masaki alisema
Mwinzala Sekele mwenye umri wa kati ya miaka 40 na 45 mkazi wa kitongoji cha Chang’ombe
kilichopo kijijini Mshewe wilayani Mbeya aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali
za mwili wake na kundi la wananchi walioamu kujichukulia sheria mkononi.
Alisema mwili wa marehemu ulikutwa saa Januari 26
mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi ukiwa umetelekezwa kijijini mshewe kata ya
Bonde la Usongwe wilayani Mbeya.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda Masaki inadaiwa kuwa
chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi kufuatia marehemu kutuhumiwa kuhusika
na mauaji yaliyotokea awali Januari 24 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri
ambapo mkazi wa mkazi wa kijiji cha Mshewe Sekela Kaini alikutwa ameuawa na
mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi kijijini hapo.
Wakati huo huo mkazi wa Ilomba jijini Mbeya Joshua
Mwaisanila(35) alifariki dunia baada ya kugongwa na lori lenye namba T 189 BLKs
Semi Trailler lililokuwa na tela lenye namba
T 193 BLK lililokuwa likiendeshwa na Ahazi Cheyo(24) mkazi wa Iyunga
jijini Mbeya.
Kaimu kamanda Masaki alisema ajali hiyo ilitokea
Januari 26 mwaka huu saa tatu asubuhi maeneo ya Forest barabara kuu ya
Mbeya/Tunduma na dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi wakati chanzo cha
ajali kinachunguzwa.
No comments:
Post a Comment