HABARI KAMILI
MSAADA wa shuka wenye thamani ya takribani shilingi milioni tano umetolewa
na Chuo cha Biashara(CBE) kwa hospitali ya Rufaa Mbeya kitengo cha wazazi na
watoto cha Meta.
CBE imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
yake ya kutimiza jumilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini
ikiwa ni wakati pia ambapo inajivunia mafanikio yake yakiwemo kusambaza matawi
yake mikoani likiwemo la Mbeya.
Akikabidhi msaada huo leo,mkuu wa chuo cha CBE Prof
Emmanuel Mjema amesema chuo kinathamini huduma za afya hudusani kitengo cha
uzazi kutokana na kuwa kati ya maeneo muhimu yanayowezesha afya ya binadamu kuimarika.
Amesema kutolewa kwa shuka hizo kunadhihirisha wazi
kuwa CBE inakijali kizazazi kilichopo na kijacho hivyo kuna kila sababu ya
kuweka mazingira bora kwa mtoto anayezaliwa ili akue akiwa na afya bora na
hatimaye maishani mwake kuja kuwa mtaalamu wa biashara akiwa miongoni mwa wadau
wa chuo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa hospitali ya wazazi Meta
Dk.John Francis amesema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani licha ya
hospitali ya rufaa katika kitengo hicho kutokuwa na uhaba mkubwa wa vitendea
kazi,bado vifaa vilivyopo havitoshelezi mahitaji.
Dk.Francis amesema kumekuwepo na ongezeko kubwa la
akina mama na watoto wanaofika hospitalini hapo kuhitaji huduma za afya hivyo
wadau wanapaswa kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali ili huduma bora
inayotolewa izidi kuwa endelevu.
No comments:
Post a Comment