Mwenyekiti wa kikundi cha Save Orphans Redson Kaisi akizungumza jambo kabla ya kukabidhi msaada
Mkuu wa kituo Malezi ya Huruma Anna Kasile akibainisha namna watoto waishio kituoni hapo wanavyopokelewa na kulelewa.
HABARI KAMILI
KIKUNDI cha Save Orphans cha jijini Mbeya kimetoa
msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima
cha Malezi ya Huruma kilichopo Simike jijini hapo.
Baadhi ya vitu vilivyokabidhiwa ni
mchele,sukari,nyama,mafuta ya kupikia na ya kupakaa,sabuni za unga na za
mche,madaftari na kalamu za wino na risasi.
Mwenyekiti wa kikundi cha Save Orphans Redson Kaisi
amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha watoto kituoni hapo
kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya kwa furaha kama ilivyo kwa watoto wengine.
Kaisi alisema kikundi hicho chenye wanachama wanne
kimekuwa kikitoa misada kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima kutokana
na kutambua mahitaji ya watoto hao ambao baadhi ya wanajamii wamekuwa
wakiwatenga.
Ameitaka jamii kwa namna inavyoguswa kujitolea
kuwasaidia watoto yatima ili kuwawezesha kuishi maisha mazuri na kutimiza ndoto
zao kwa kuwajengea mazingira bora ya kuishi.
“Asilimia kubwa ya jamii tumekuwa tukijisahau kwa
kuwapa huduma za msingi watoto tunaoishi nao majumbani pekee.Tunasahau kuwa
wapo ambao hawana wazazi wala walezi ambao nao wana uhitaji kama wale tunaoishi
nao.Tukiendelea kuwasahau tujue tunajenga tabaka la kiubaguzi ndani ya jamii
zetu” alisema Kaisi.
Akipokea msaada huyo,mkuu wa kituo Malezi ya Huruma Anna
Kasile amesema amekuwa akiwalea watoto kituoni hapo katika mazingira magumu
kutokana na kutokuwa na chanzo cha mapato zaidi ya misaada ya wadau mbalimbali.
Kasile pia amelalamikia uwepo wa watu ambao wamekuwa
wakimbeza kwa kumuita mtu aliyepungukiwa na akili na ndiyo sababu anaendelea
kupokea na kuishi na watoto waio wake.
Hata hivyo amesema changamoto hizo haziwezi
kumkatisha tama,badala yake anazichukulia kama chanhu ya kuongeza upendo wake
kwa jamii ya watoto yatima na kuomba wadau zaidi kuendelea kushirikiana naye
katika kutimiza malengo na ndoto za watoto kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment