Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo
ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa
makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro,
Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan
Dau.
Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa
vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi
Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro
ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga
ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara
ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz
Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa
kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato
Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na
ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya
Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti
(Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari,
2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016
No comments:
Post a Comment