WANAFUNZI 95 katika shule ya
sekondari ya wavulana ya Iyunga jijini Mbeya hawana mahali pa kulala kufuatia
moto mkubwa kuteketeza Bweni lao leo (Feb 29) lililokuwa likifahamika kwa jina
la Mkwawa.
Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo Edward
Mwantimwa moto huo umezuka majira ya saa 4:00 asubuhi wakati wanafunzi
wakiwa darasani wakiendelea na masomo na baadaye Askati wa Jeshi la
Zimamoto na uokoaji walifika na kufanikiwa kuuzima ukiwa umeteketeza bweni lote.
Mwantimwa amesema pamoja na
kutokuwepo kwa mwanafunzi aliyejeruhiwa moto huo umeteketeza vifaa mbalimbali
vikiwemo vitanda,magodoro na nguo za wanafunzi 95 waliokuwa wakilitumia bweni
hilo huku bweni jirani la Nyerere likiadhiriwa kidogo pia.
Akizungumzia chanzo cha tukio
hilo,mkuu huyo wa shule moto amesema umetokana na hitilafu ya umeme kwenye
soketi ambayo ipo karibu na mlangoni lakini hakubainisha iwapo soketi hiyo
ilikuwa ikitumika wakati tukio likitokea.
Amesema kutokana na moto kuanzia
katika eneo la mlango ilikuwqa vigumu kwa waokoaji kuweza kuingia ndani na
kuokoa vitu vilivyokuwemo.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Nyirembe Munasa amesema sababu ya moto huo ni uchakavu wa
miondombinu ya shule hiyo kongwe iliyojengwa tangu wakati wa utawala wa
Mkoloni.
Munasa amesema kutokana na uchakavu
wa majengo wanafunzi pamoja na watumishi shuleni hapo wanapaswa kuchukua
taadhari katika utumiaji wa miundombinu hiyo hasa ya umeme, vyoo, na maji
ambayo inaokena inauchakavu mkubwa.
Mkuu huyo wa wilaya amemtaka kaimu
mkurugenzi wa halmaashauri ya jiji la Mbeya Dk Samwel Lazaro kununua
vifaa muhimu kwa mahitaji wa wanafunzi wakati mpango wa kukarabati jengo la
bweni lililoungua ukiendelea kufanyiwa kazi.Thamani halisi ya hasara iliyopatikana bado haijafahamika.
No comments:
Post a Comment