MWENENDO mbaya wa timu ya Mbeya City katika ligi kuu
Tanzania bara umeonekana kuwachanganya wadau wa soka mkoani hapa kiasi cha
kuanza kuutupia lawama uongozi wa timu hiyo sambamba na Chama Cha Soka mkoa wa
Mbeya(MREFA).
Katika maeneo na nyakati tofauti wadau hao
wameelezea masikitiko waliyonayo juu ya mweneno wa Mbeya City huku wakisisitiza jitihada za haraka
kufanyika ili kuinusuru timu hiyo kushuka daraja.
Baadhi ya wadau wanasema matokeo mabovu kwa michezo
ya timu hiyo inatokana na usajiri mbovu,wengine kushuka kwa nidhamu ya
wachezaji ni chanzo huku wengine nao wakisema kutokuwepo kwa maelewano baina ya
uongozi wa timu na Mrefa ni tatizo.
“Tunashangaa timu inafanya vibaya viongozi wako
kimya hatuoni hamasa yoyote iliyo shirikishi ili kutafuta ufumbuzi.” Alisema mmoja
wa wadau hao Godfray Davis
Naye Mwalimu Josephat Antony amesema jitihada za
dhati za haraka zinapaswa kufanyika ili kuinusuru Mbeya City akisema
kuipandisha timu inaposhuka daraja ni kazi kubwa hivyo ni muhimu kutoruhusu
hali hiyo kutokea.
Kwa upande wake Edward Mwambusye amesema kusajiri
wachezaji wakongwe ndiyo kunakoiponza Mbeya City kwakuwa wachezaji hao
wanajioni fahari na hivyo hawaoni sababu ya kujituma wawapo uwanjani.
Anasema kinachotakiwa kwa sasa ni wadau kuona
uwezekano wa kuikoa timu hiyo isishuke daraja lakini matokeo yanayopatikana
yawe fundisho kwa timu hiyo katika msimu mwingine wa usajiri.
Akizungumzia suala la ushirikiano baina ya Mrefa na
uongozi wa Mbeya City,katibu wachama hicho cha soka mkoa wa Mbeya Seleman
Haroub amesema si kweli kuwa pande hizo haziwasiliani na badala yake akasema
ipo mikakati mbalimbali inayofanyika ili timu hiyo isishuke daraja.
Haroub amesema aliwahakikishi wadau wa soka ndani na
nje ya mkoa wa Mbeya kuwa Mbeya City haitashuka daraja na mkakati uliopo hivi
sasa ni kuhakikisha kila mchezo inaocheza inaibuka na pointi tatu zote.
No comments:
Post a Comment