Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 2, 2013

Mwanamke mmoja anashikiliwa na polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumuuza mtoto wa kaka yake ili aweze kupata fedha kwaajili ya kusaidia katika kesi ya kaka yake. Mwanamke huyo amefahamika kwa jina la Tabu Mwashipete(40) mkulima na mkazi katika kijiji cha Mpemba wilayani Momba mkoani hapa. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman alisema mwanamke huyo alikamatwa juzi(Aprili mosi) majira ya saa 2:00 usiku na kumtaja mtoto aliyekuwa akiuzwa kuwa ni Hosea Mwashipete(5). Kamanda Athumani alisema mwanamke huyo alikuwa akimuuza mtoto Hosea kwa mkazi mwenzake wa kijiji cha Mpemba John Sinyinza(64) kwa gharama ya shilingi 1,000,000. Alisema sababu ya kuuzwa kwa mtoto huyo ni kutafuta fedha kwaajili ya kusaidia katika kesi inayomkabili baba wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Simon Mwashipete anayekabiliwa na kesi ya mauaji nchini Malawi. Kamanda huyo amemtaja mteja wa biashara hiyo ndiye aliyewezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa kwani akiwa amemlipa fedha ya awali kiasi cha shilingi 100,000 alitoa taarifa polisi na kisha kuweka mtego uliowezesha kumkamata mwanamke huyo wakati wakiendelea kufanya mazunguzo ya lini atamalizia kiasi cha shilingi 900,000. Kwa mujibu wa Athuman mama wa mtoto huyo alikwisha fariki dunia hivyo Hosea amekuwa akiishi nyumbani kwa shangazi yake aliyeamua kumuuza ili kupata kiasi hicho cha fedha.

No comments:

Post a Comment