Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, April 24, 2013

MAUAJI TENA

MAUAJI yatokanayo na imani za kishirikina yamezidi kuugubika mkoa wa Mbeya na sasa hali inatisha na kuhitaji uwepo wa mikakati ya ziada kupambana na hali hiyo. Siku chache baada ya watu watatu kuuawa kwa imani za kishirikina akiwemo mfanyakazi wa reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) Ambrose Lucas aliyedhaniwa kuwa na lengo la kuiba watoto mtu mwingine pia ameuawa akituhumiwa kuwa mchawi. Aliyeuawa safari hii amefahamika kwa jina la Laison Mjaha(78) mkulima na mkazi wa kijiji cha Mawelo wilayani Chunya mkoani hapa. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki amesema kifo cha Laison kilibainika jana saa 4:00 asubuhi baada ya kukutwa akiwa ameuawa kwa kupigwa na sululu kwenye paji la uso wake nyumbani kwake. Alisema mbinu iliyotumika ni wauaji ambao hadi sasa hawajafahamika kumvamia mkazi huyo alipokuwa amelala nyumbani kwake na kasha kumtendea unyama huo kwa njia ya kujichukulia shetia mikononi. Masaki amesema mauaji hayoyanahusishwa na imani za kishirikina kwakuwa kwa muda mrefu marehemu alikuwa akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment