Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, April 6, 2013

WATANZANIA WATAKIWA KUJIVUNIA KUMILIKI ZIWA NYASA

TANZANIA huchangia asilimia 59 ya maji ya ziwa Nyasa kupitia mito yake kiasi ambacho ni kikubwa ikilingaanishwa maji kutoka nchi za Malawi na Msumbiji. Hayo yalibainishwa na Ofisa wa maji Bonde la ziwa Nyasa Witgal Nkondola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Nkondola amesema nchi jirani ya Malawi inachangia asilimia 33 ya maji ya ziwa hilo huku asilimia nane zinazosalia zikichangiwa na mito iliyopo nchini Msumbiji. Hata hivyo ofisa huyo amesema ni watanzania wachache wanaotambua kuwa mitoaa yao inachangia kwa kiasi kikubwa maji ya ziwa hilo hivyo wanapaswa kujisikia fahari kuwa sehemu ya wamiliki wa ziwa hilo. Almeitaja mito ya Songwe,Kiwira na Lufilyo iliyopo mkoani Mbeya kuwa miongoni mwa mito inayoingiza maji kwa wingi katika ziwa hilo. Amekiri pia vivutio vya utalii vilivyopo kwenye ziwa hilo na eneo zima la Bonde la Maji la Ziwa Nyasa kutotangazwa ipasavyo yakiwemo maziwa madogo ya asili 11 yaliyopo wilayani Rungwe.

No comments:

Post a Comment