Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 23, 2013

TBC YAAHIDI UELEDI KATIKA UTENDAJIKAZI WAKE

SHIRIKA la Utangazani la TBC limeahidi kuendelea kuwatumikia watanzania kwa kuwapa habari zilizoandaliwa kwa umakini na weledi wa hali ya juu. Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitugine alitoa ahadi hiyo katikaa semina ya wadau wa uandaaji wa vipindi vya shirika hilo iliyofanyika jijini Mbeya. Kitugine alisema ni wajibu wa TBC kuwatumikia wananchi ambao ndiyo walingwa hasa wa kuanzishwa kwa shirika hilo tangu awali. “Tuna tambua kuwa taifa linategemea sana shirika letu.Ndiyo sababu wakati wote tunafanya kadiri tuwezavyo ili tuweze kuwatumikia watanzania kwa kuwahabarisha juu ya mambo mbalimbali yanayotokea na kuendelea nchini.Kama ilivyo kwa vyombo vya habari vingine TBC ina wajibu wa kufanya shughuli zake kwa umakini mkubwa hasa kwa kutambua kuwa inabeba sura ya taifa.Ni kwa kulitambua hilo kila mara tunawasisitiza waandishi wetu wa habari kujikita katika uibuaji wa changamoto na pia maoni yenye kuleta suluhu kutoka kwa wadau”. Alisema Hata hivyo Kitugine alisema zipo changamoto mbalimbali zinazoukabili utendaji kazi wa TBC ikiwemo uhaba wa vifaa na pia bajeti finyu isiyotosheleza mahitaji ya uendeshaji wa shirika hilo. Lakini alisema changamoto hizo haziwavunji moyo wa kuendelea kuwatumikia watanzania kwa kuwahabarisha,kuwaelimisha na kuwaburudishaa kupitia vipindi mbalimbali vya vituo vya redio na televisheni vinavyomilikiwa na shirika hilo la kiserikali. Akifunga semina hiyo mkurugenzi wa kitengo cha usalama wa chakula kutoka mamlaka ya usimamizi wa ubora wa Chakula na Dawa nchini(TFDA) Raymond Wigenge aliwataka waandishi wa habari wa TBC kujikita kwenye uandaaji wa vipindi vya kijamii vilivyo bora ili kupambana na adui ujinga,maradhi na umasikini. Alisema kwa kuwa na vipindi vya kupambana na maadui hao tasnia ya habari nchini itakuwa yenye manufaa kwa umma tofauti na vipindi vya uchonganishi vinavyoibua chuki ndani ya jamii na kuwa kikwazo cha maendeleo. Wadau waliohudhuria semina hiyo ni pamoja na maafisa kutoka TBC,TFDA na taasisi za elimu ya juu nchini.

No comments:

Post a Comment