Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 23, 2013

WAWILI WAUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MBEYA

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio ya mauaji tofauti yaliyotokea mkoani Mbeya kutokana na imani za kishirikina. Tukio la kwanza la mauaji lilitokea juzi majira ya saa 3:00 usiku katika kitongoji cha Katumba kijijini Ndala kata ya Kandete wilayani Rungwe ambapo mkazi wa kijiji cha Lusasi kata ya Mpombo Lufingano Nsinge(32) aliuawa na wananchio walioamua kujichukulia sheria mkononi. Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki chanzho cha mauaji hayo ni wananchi hao kumtuhumu Lufingano kuwa mhusika wa mauaji ya watoto wadogo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara kwenye maeneo hayo. Masaki alisema kabla ya kuuawa na wananchi,Lufingano alikutwa ndani ya nyumba ya mtu aliyefahamika kwa jina la John Mwasamaleba(53) mkazi wa kijiji cha Ndala ambako ilisaidikiwa aliingia ndani ya nyumba hiyo akiwa anamvizia mmoja wa watoto wa nyumba hiyo ili afanye mauaji. Baada ya wananchi kujikusanya walianza kumpiga mtu huyo kwa kutumia silaha za jadi yakiwemo mapanga,vipande vya kuni,shoka na mipini hadi alipopoteza uhai wake. Kaimu kamanda huyo alisema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu watu wane akiwemo mwenye nyumba alimokutwa marehemu kabla ya kuuawa na wananchi. Wengine ni Angolisye Mwakalinga(30),Lucas Mwasamaleba(40) na Leah Ndemange ambaye hakufahamika umri wake mara moja lakini wote hao ni wakazi wa kijiji cha Ndala wilayani Rungwe. Katika tukio la pili lililotokea majira ya saa 7:00 ya usiku wa kuamkia jana(April 23) katika kijiji cha Chobwe wilayani Ileje,Anna Panja(60) aliuawa kwa kuchinjwa shingoni kwa kisu na watu wawili akiwemo mwanaye wa kumzaa. Kaimu kamanda Masaki alimtaja mtoto wa marehemu aliyehusika na mauaji ya mama yake kuwa ni Michael Panja ambaye akiwa na mwenzake asiyefahamika jina walimvamia mama yake aliyekuwa amelala na baba wa familia Basale Panja(76) na ndipo wakamuua kwa kumchinja shingo kwa kisu kabla ya kukimbilia kusikojulikana. Kwa muda mrefu Michael alikuwa akimtuhumu mama yake kuwa mchawi ambaye amekuwa akimloga mkwewe ambaye ni mke wa moto huyo.

No comments:

Post a Comment