Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, April 3, 2013

VURUGU ZA TUNDUMA 40 MBARONI

MJI mdogo wa Tunduma wilayani Momba jana haukuwa shwari kufuatia vurugu zilizoanzishwa na kikundi cha baadhi ya wakazi huku zikihusishwa na itikadi za kidini katika suala zima la uchinjaji. Vurugu hizo zilizuka majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya waanzilishi wa vurugu hizo kuingia katika barabara kuu na kuanza kuchoma magurudumua ya magari huku pia wakiweka mawe makubwa barabarani. Hata hivyo chanzo cha vurugu hizo kilionekana kupokelewa kwa mitazamo tofauti ambapo wapo baadhi walionekana kupinga kuwa zinahusisha masuala ya kidini kwakuwa walioonekana kushiriki ni vijana wapiga debe walioonekana kuchanganyikana na vibaka. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa muda mpaka kati ya Tanzania na nchi jirani ya Zambia kwa hofu ya usalama,shugjhuli za kibiashara zilisimama huku pia mabasi ya abiria kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa yakizuia kuendelea na safari hadi alipofika kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman. Akizungumzia tukio hilo kamanda Athuman alisema wni vigumu kusema moja kwa moja vurugu hizo zina msukumo wa itikadi za kidini ama la kwakuwa washiriki ni watu wanaonekana kupenda kutumia vurugu kujinufaisha kwa kuiba. “Tunduma kuna watu wamejenga mazoea ya wao kuonekana kama ndiyo wapenda vurugu.Wao bila kuwepo kwa vurugu hawasikii raha.Lakini pia wanaonekana kuwa na maslahi kupitia migogoro hiyo na ndiyo sababu wamekuwa wakianzisha chokochoko za kuchafua amani kila wakati”. “Leo makundi ya waharifu wameingia barabarani na wakiwa pia wanarusha mawe hovyo kwa askari waliokuwa wamejipanga kukabiliana na hali hiyo hivyo ikalazimu askari kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya wahalifu hao” Kamanda huyo alisema athari zilizotokana na vurugu hizo ni pamoja na kujeruhiwa kwa askari mmoja wa jeshi hilo baada ya wafanya vurugu kurusha mawe na kuvunja kioo cha gari ya polisi aliyokuwa akiendesha. Alisema pia kutokana na kurusha mawe hovyo wafanya vurugu walimjeruhi mwenzao mmoja ambaye alikimbizwa hospitali na kuanza kupata majeruhi. Athari ni nyingine ni kuvunja msikiti mmoja kuvunjwa na wavunjaji kutaka kuondoka na madirisha ya jingo hilo lakini wakakimbia na kuyaacha baada ya polisi kufika eneo hilo. Kamanda Athuman alisema pia nyumba ya askari mmoja ilivamiwa na kuvunjwa dirisha moja lakini kutokana na eneo hilo kuwa na mbwa wengi walifunguliwa na kuwakurupusha. Kwa mujibu wa kamanda huyo zaidi ya watu 40 walikamatwa na jeshi hilo kwaajili ya kuhojiwa juu ya tukio hilo huku pia akisisitiza hatua za kisheria kuchukuliwa kwa mtu yeyote atakayekuwa amehusika pasipo kujali ni katika itikadi ya kidini au siasa. Aliwataka wakazi katika mji wa Tunduma na mkoa wa Mbeya kwa ujumla kutokubaliana na watu wachache wanaopenda kuvuruga amani kwa lengo la wao kujinufaisha.

No comments:

Post a Comment