WAKAZI wa vijiji vilivyopo katika kata ya Mtanila
wilayani Chunya wameonesha nia ya kweli ya mahitaji ya umeme wakisema
wamejiandaa kunufaika nao mara tu utakapofikishwa kijijini hapo.
Tayari serikali kupitia wakala wa Umeme vijijini(Rea)
imefikisha nyaya za umeme kwenye vijiji vya kata hiyo na kuna kila dalili za
nishati hiyo kuanza kugawanywa kwa wananchi hivi karibuni.
Miongoni mwa vijiji vilivyofungiwa tayari nyaya za
umeme ni Igangwa ambapo wakazi wake wanasema hivi sasa wanaomba usiku na mchana
shughuli za ufungaji huo zikamilike mapema ili waanze kunufaika kama ilivyo kwa
maeneo mengine nchini.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Igangwa Hamis Mwandura
alimwambia mwandishji wetu kuwa wakazi wana shauku kubwa ya kuanza kutumia
umeme kwakuwa wamechoshwa na matumizi ya nishati mbadala vikiwemo vibatari,taa
za kandiri na mishumaa.
Kijana Hamisi alisema kwa kukosekana kwa umeme
kijiji cha kimeendelea kusuasua kimaendeleo kwakuwa shughuli nyingi hivi sasa
zinahitaji nishati hiyo ili kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Alisema kwa sasa njia pekee inayotumika kuwasaidia
wakazi wa kijiji hicho na vingine vya jirani katika kupata mwanga nyakati za
usiku na pia kuchaji simu ni umeme wa nishati ya jua aliosema kimsingi
hautosjhelezi mahitaji yaliyopo.
“Sola zinatusaidia kuchaji tu simu na kupata mwanga
kwa taa chache nyakati za usiku.Umeme huu hauna msaada mkubwa sana kwetu
kwakuwa hata sola zenyewe tunazofunga ni ndogo.Tunahitaji umeme wa uhakika
kuendesha shughuli zetu ili tuharakishe kupata maendeleo”
“Tunaamini tukipata umeme tutaweza kufanya mambo
mengi.Biashaza za vinywaji zitafanyika zaidi kutokana na uwepo wa hali ya joto
katika maeneo yetu.Tutaweza pia kufuga kuku kwa njia za kisasa tofauti na sasa”
alisisitiza Hamis.
No comments:
Post a Comment