Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, November 30, 2015

PATA KITUKO HIKI CHA MZARAMO V/S MCHAGA

Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote kwa tsh. 100,000/= Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki yako nakukuongeza laki nyingine. MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.

MZARAMO: "unaumwa nini?" 

MCHAGA: "Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa.." 
MZARAMO: "sawa, toa laki kabisa.." Mchaga akatoa. 
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; "Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu.." 
MCHAGA akanywa akatema faster; "Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?" 
MZARAMO: "Umepona karibu tena.." Mchaga aka-mind sana

Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake. MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau sanaaaaa.." MZARAMO akamwambia "hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..' MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..' 
MZARAMO: "nesi naomba kikopo no.27.."
MCHAGA: "ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?" 
MZARAMO: "UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.

No comments:

Post a Comment