HOSPITALI ya Rufaa kanda ya Mbeya,imetoa namba
maalumu za simu za kiganjani zitakazotumika kwaajili ya taarifa za msaada wa dharula lengo likiwa ni kurahisisha
mawasiliano baina ya taasisi hiyo na jamii.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk.Mpoki Ulisubisya amesema
kwa Makao makuu ya hospitalini hiyo itatumika 0767 314 250 wakati kitengo cha
wazazi Meta itatumika namba 0755 333 574.
Anasema kuwekwa kwa huduma ya simu kwaajili ya
wateja ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Katibu mkuu wizara ya
Afya na ustawi wa jamii Dk.Donan Mmbando alipofanya ziara hospitalini hapo hivi
karibuni.
“Sisi tumeona tuanze kutekeleza maagizo tuliyopewa
mapema kabisa.Hakuna sababu ya kusubiri tena.Tunahitaji kwenda sambamba na kasi
ya uongozi uliopo madarakani ya Hapa kazi tu” anasema Dk.Ulisubisya.
Anasema kuanzisha kwa huduma hiyo kutawezesha
ndugu,jamaa na marafiki kupata taarifa sahihi juu ya ndugu zao watakaokuwa
wamelazwa kwenye hospitali hiyo kwaajili ya huduma za kimatibabu.
Hata hivyo anasema namba hizo mbili zitatumika kwa
muda na ukomo wake utakuwa mara tu baada ya kampuni za simu kutengeneza namba
maalumu ambayo mteja wa hospitali atapiga simu pasipo kutozwa gharama zozote.
Alisema tayari uongozi umekwisha wasilisha ombi la
kutengenezewa namba hizo maalumu kwenye kampuni moja ya simu na uongozi wa
kampuni husima umeridhia kutengeneza namba hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wateja hospitalini hapo
wamezungumzia mpango huo kuwa muhimu kwakuwa utawezesha jamii kupata taarifa na
majibu sahihi juu ya maswali wanayokuwa wakijiuliza hususani yanapotokea
matatizo kama ya ajali na miili ya watu waliopoteza maisha na majeruhi
kupelekwa kwenye hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment