JITIHADA
za kuokoa wachimbaji wawili waliofukiwa na kifusi katika machimbo bubu ya
dhahabu yaliyopo eneo la mnadani kata ya Sangambi, wilayani Chunya zimeendelea
tena jana jumanne(Disemba 29) na hatimaye kuzaa matunda kwa mmoja wa wakichamji
hao kuopolewa akiwa amefariki dunia.
Wachimbaji
madini hao walifukiwa na kifusi tangu Disemba 27 mwaka huu majira ya asubuhi na
shughuli ya kufukua kifusi ili kuwaokoa ikaanza Disemba 28 majira ya asubuhi
baada ya mashine ya kufukua kifusi kupatikana.
Hata
hivyo kutokana na gari lenye mashine hiyo kutokuwa na taa ililazimu shughuli
hiyo kusitishwa ilipofika juzi jioni na kiza kuanza kutanda hivyo shughuli hiyo
ikaendelea tena jana Disemba 29.
Akizungumza
na Lyamba Lya Mfipa kutoka eneo la tukio,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Chunya Bosco Mwanginde amesema jitihada za ufukuaji kifusi zilianza kuzaa
matunda majira ya saa nane mchana baada ya wananchi waliokuwepo kufanikiwa
kuopoa mwili wa mmoja wa wachimbaji hao.
Mwanginde
amemtaja marehemu ambaye mwili wake uliopolewa jana kuwa ni Wambula Makulu
mwenyeji wa Musoma mkoani Mara aliyesema alihamia maeneo hayo miaka kadhaa
iliyopita.
Mwanginde
amesema pamoja na kuukuta mwili huo shughuli ya kufukua kifusi iliendelea kwa
lengo la kumtafuta mchimbaji mwingine aliyemtaja kwa jina la Riziki Kalengo
mkazi wa wilayani Mbozi japo pia jioni shughuli hiyo ilisimama na imeendelea leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment