HOFU
ya kusambaa kwa ugonjwa wa Kipindupindu imezidi kutanda mkoani Mbeya licha ya
kuwa mkoa huo ni moja kati ya maeneo nchini yaliyoanza kutekeleza mapema agizo
la Usafi lililotolewa na Rais John Magufuli.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amethibitisha kuwepo kwa taarifa za wagonjwa wa
kipindupindu katika kambi ya Lema wilayani Kyela.
Kandoro
amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo alipokuwa akiwahamasisha wakazi wa mji mdogo
wa Mlowo wilayani Mbozi huku akiwahimiza kuzingatia suala la usafi ili
kuepukana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Amesema
tayari wagonjwa 27 wa kipindupindu wameripotiwa na wamehifadhiwa katika kambi
ya kijiji cha Lema waanakoendelea kupatiwa matibabu lakini tayari wawili kati
yao wamefariki.
“Awali nilidhani mimi nimepona kupata
kipindupindu lakini hadi muda huu ninapoongea na nyie nimepata taarifa ya
wagonjwa 27 walioko katika kambi ya kijiji cha Lema wilayani Kyela na kati yao
wawili wamefariki dunia” anasema Kandoro.
Anasema
awali waliripotiwa wagonjwa 9 ambapo kati yao 1 alifariki na wengine 7 walipata
matibau na kuruhusiwa kurudi nyumbani huku mmoja akiendelea na matibabu kambini
hapo kabla idadi hiyo haijaongezeka.
Amesema
njia pekee ya kuepuka ugonjwa huo ni kwa wakazi wa maeneo yote ya mkoa wa Mbeya
kuhakikisha wanazingatia usafi huku akisema pamoja na maeneo mengi wananchi
kuitikia kwa kasi dhima ya kufanya usafi bado kuna changamoto ya kuwabadili
wananchi kuwa na tabia ya kufanya usafi katika mazingira yao.
No comments:
Post a Comment