Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, December 5, 2013

KANISA LA ANGLIKANA LAKABIDHI PIKIPIKI ZA KUENDESHEA MRADI WA PAMOJA TUWAJALI

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za juu kusini,John Mwela akikabidhi pikipiki aina ya Yamaha kwa afisa Ustawi wa jamii wa jiji la Mbeya Bupe Joel kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwajali unaoendeshwa na kanisa hilo katika kata 16 kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji hilo. TAASISI za kidini mkoani Mbeya zimepewa wito wa kushirikiana na serikali katika utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo suala la malezi ya watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi. Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za juu kusini,John Mwela alitoa changamoto hiyo alipokuwa akikabidhi pikipiki mbilia aina ya Yamaha kwa wasimamizi wa mradi wa Pamoja Tuwalee unaoratibiwa na kanisa hilo na unaendeshwa katika kata 18 kati ya 36 zilizopo jijini Mbeya. Moja ya pikipiki hizo zilizotolewa na shirika la Pact Tanzania,ilikabidhiwa kwa mratibu wa mradi kupitia kanisa na nyingine kwa halmashauri ya jiji la Mbeya ambayo nayo kwa upande wake inashiriki bega kwa bega kutekeleza mradi huo. Akikabidhi pikipiki hizo,askofu Mwela alisema taasisi za kidini hazipaswi kuishia kueneza neon la Mungu pekee badala yake ni zinapaswa kujikita pia kushiriki katika kuhakikisha jamii iliyopo inakuwa salama na yenye maisha bora. “Ni muhimu tukawa pamoja katika kuisaidia jamii inayoteseka.Kuwatekeleza mradi unaohusika na watoto waishio kwenye mazingirahatarishi si ndogo.Lakini sisi kama kanisa tutaendelea kushirikiana na serikali kuisaidia jamii yetu.” Alisema. Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Mbeya katika kupokea moja ya pikipiki hizo,afisa ustawi wa jamii Damas Mlwale alisema jiji la Mbeya linakabiliwa na changamoto kubwa ya uwepo wa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu. Mlwale alisema mikakati ya pamoja kati ya serikali na wadau wengine inahitajika kwa kiasi kikubwa katika kutafuta suluhisho la changamoto hiyo hivyo kupewa pikipiki ni moja ya njia za kupunguza ukubwa wa tatizo kwakuwa itarahisisha kuwafikia watoto mahali walipo. Naye Mkurugenzi wa maendeleo ya Dayosisi Padre Jonathan Mwashilindi ambaye ndiye mratibu wa mradi huo wa miaka miwili na nusu alisema serikali bado inamzigo mkubwa wa kuiletea jamii maendeleo. Alisema kupitia mradi huo jumla ya dola za kimarekani 46,606 zimetolewa na Pact Tanzania na zitatumika katika kipindi cha oktoba 2013 na Septemba 2014.

No comments:

Post a Comment