Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, December 2, 2013

MEYA NA MBUNGE WOTE WA CCM WASHUSHUANA KWENYE KIKAO

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga akizungumza kwa hisia kupinga wazo alilolitoa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Mary Mwanjelwa kwenye kikao cha balaza la Madiwani wa halmashauri ya jiji Mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa aliposimama awali na kuzungumza kwa hisia kwenye kikao cha balaza la Madiwani Baada ya Madiwani wa Chadema kutaka watuhumiwa wa ufisadi ndani ya halmashauri hiyo watajwe kwenye kikao lakini Mstahiki Meya akakataa na kufafanua kuwa kanuni haziruhusu watumishi watumumiwa kujadiliwa katika balaza hadi pale balaza linapojigeuza na kuwa kamati. Lakini Mbunge Dk.Mwanjelwa alisimama na kusema kufanya hivyo kunasababisha madiwani kuonekana hawana meno na kubainisha kuwa mbona bungeni wabunge huwaita mawaziri husika na kuwahoji.Hapo ndipo Mstahiki Meya Kapunga alipotumia nafasi yake kumjibu mbunge huyo hali iliyodhihirisha kuwa kwa kauli ya mbunge ni wazi anauunga mkono upande wa upinzani ulioonekana kujipanga zaidi katika jambo hilo hali iliyosababisha kuwepo kwa ulinzi mkali kila kona ya eneo la kituo cha mikutano cha Mkapa kilichopo sokomatola Hapa si bungeni,na masuala ya bungeni yaache huko huko!Aliongea Kapunga kwa sauti kali na kuendele........Mimi siendeshi vikao vya balaza kwa kanuni za bunge bwana!Nimesema haiwezekani kumvua nguo humu!Huo utaratibu wa bungeni ni wenu huko huko. Baadhi ya madiwani na wakuu wa Idara mbalimbali wakifuatilia malumbano hayo ya muda mfupi kati ya Mbunge na Meya wote wakiwa ni wa Chama Cha Mapinduzi(CC,).

No comments:

Post a Comment