Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, December 13, 2013

WAWILI WAFA MBEYA

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwamo la mtoto kufa maji wakati akiogelea na wenzake mtoni. Mtoto aliyekufa maji amefahamika kwa jina la Zela Mnenwa mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa kijiji cha Mahango wilayani Mbarali. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman alisema tukio hilo lilitokea jana(Desemba 12) saa 8:30 mchana katika mto Lyandembela ambapo akiwa anaogelea na watoto wenzake ambaio hakuwataja majina mtoto huyo alizidiwa na maji na kufariki dunia kwa kumezaa maji mengi. Katika tukio la pili dereva aliyefahamika kwa jina Heriel Mzava(38) mkazi katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro amefariki dunia papo hapo baada ya gari lenye namba T 336 ATL aina ya Mitsubish Fuso aliyokuwa akiendesha kuigonga kwa nyuma gari yenye namba T 385 BYA aina ya Mitsubish Fuso pia iliyokuwa ikiendeshwa na Yona Mwakibenga(34) mkazi wa Mwanjelwa jijini Mbeya. Kamanda Athuman alisema ajali hiyo ilitokea jana(Desemba 12) majira ya saa maeneo ya Uyole jijini Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tukuyu ambapo pia kondakta wa fuso namba T 336 ATL aliyemtaja kwa jina la Omary Salimin(22) mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro alijeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya. Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliomshinda dereva wa fuso yenye namba T 336 ATL na kulazimika kugonga kwa nyuma fuso iliyokuwa mbele yake kabla hajapoteza maisha papo hapo.

No comments:

Post a Comment