Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 3, 2013

ZIARA YA WAJUMBE WA DAWATI LA KUPINGA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA LA POLISI MBEYA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA MSAMARIA MWEMA

Mmoja wa wajumbe wa dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya Mary Gumbo akikabidhi zawadi ya sabuni kwa watoto yatima waishio katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya.Wajumbe wa dawati hilo wapo katika ziara ya kutembelea vituo mbalimbali ikiwa ni katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kiijinsia JAMII ya watoto yatima imeshauriwa kutokatishwa tama na maisha magumu yanayoikabili badala yake iendelee kushirikiana na wadau wanaoijali katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili. Mkuu wa Dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya mkaguzi msaidizi wa jeshi hilo Samora Saranga aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya. Saranga aliyeambatana na wajumbe wengine wa dawati hilo kutembelea kituo hicho alisema watoto yatima wanapaswa kutambua kuwa maisha wanayoishia yapo katika mipango ya mwenyezi Mungu na si wao wala wazazi wao waliopenda jamii hiyo iishi hivyo. Ziara ya wajumbe wa dawati hilo kituoni hapo ni mwendelezo wa ziara katika vituo mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment