Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, July 24, 2012

MAANDALIZI YA SIKU YA MASHUJAA JULAI 25

Siku ya Mashujaa nchini Tanzania inaadhimishwa kesho Julai 25 ambapo Majeshi ya Ulinzi na Usalama yatakuwa yakiwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliofariki kwa ajili ya kulipigania taifa hili,pia kwenye vita kuu ya pili ya Dunia.
Kitaifa yataadhimishwa mkoani Dar es Salaam ambapo wito umetolewa kwa wakazi wa Jiji hilo kujitokeza katika maadhimisho hayo huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mkoani Mbeya mapema leo asubuhi maandalizi kwa ajili ya siku hiyo yamefanyika katika viunga vya Jiji la Mbeya karibu na eneo la Kumbukumbu ya Mashujaa.

Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama vilikuwa na kazi moja tu ya kujiandaa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Polisi  na Jeshi la Magereza.
 JWTZ KIKOSI CHA 44KJ
 JESHI LA MAGEREZA
 JESHI LA POLISI

No comments:

Post a Comment