VIONGOZI
wa dini,vyama vya siasa na asasi mbalimbali za kiserikali na
binafsi
wametakiwa kushiriki katika kutoa hamasa itakayowezesha
kufanikishwa
kwa zoezi la sense ya watu na makazi linalotarajiwa
kufanyika
agosti 26 mwaka huu.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alitoa mwito huo alipokuwa
akifungua semina ya siku 12 inayolenga kutoa mafunzo kwa
wasimamizi
wa sense watakaokwenda kuwafundisha makarani katika kata za
wolaya
zilizopo mkoani hapa.
Kandoro
alisema viongozi hao wanayo nafasi kubwa ya kutoa elimu juu ya
umuhimu
wa sense ya watu na makazi kwa jamii wanazozihudumia hivyo
wakiwajibika
ipasavyo watakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha
zoezi
hilo.
Aliwaomba
kutumia fursa walizonazo kuwaelimisha wananchi juu ya
umuhimu
huo ikiwa ni pamoja na kuiwezesha serikali kuwa na takwimu
sahihi
zitakazosaidia kuwa na mipango ya kimaendeleo inayoendana na
hali
halisi ya mahitaji iliyopo nchini.
Aliwataja
wanahaabari kupitia vyombo vyao kuwa mchango mkubwa na
muhimu
unaohitajika pia katika kutoa elimu juu ya Sensa pamoja na
kuufahamisha
umma juu ya njia mbalimbali zitakazotumika na ni jinsi
gani
taarifa zitakazotolewa na wananchi zitabaki kuwa siri.
Aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha pale makalani
watakapofika
katika familia zao na kuhitaji taarifa mbalimbali
kutokana
na kumbukumbu alizosem,a pia wanapaswa waziandae ili
kurahisisha
mahojiano baina yao.
Mkuu
huyo wa mkoa aliwataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha
wanakuwa
makini kwenye mafunzo ya nadharia na vitendo wanayopewa ili
baadaye
waende kuwa walimu wazuri kwa wenzao watakaokwenda
kuwafundisha
kwenye kata za wilaya wanazotoka.
Alisema
ni vema wakatambua kuwa taifa limewaamini na kuwapa dhamana
kubwa
likiwa na imani kuwa watatekeleza wajibu wao kwa
umakini,uadirifu
na uaminifu mkubwa ili lipate takwimu zilizo sahihi.
“Nina
imani hamkupendelewa,mliteuliwa kutokana na sifa mlizonazo.Vivyo
hivyo
na taifa linategemea mtafanya vile linavyohitaji.Zoezi hili
linaigharimu
serikali pesa nyingi lakini ni muhimu na ndiyo maana
limekuwa
likifanyika kila baada ya miaka kumi” alisema
Alisema
miaka yote zoezi kama hilo limekuwa likifanyika vizuri lakini
mwaka
huu linapaswa lifanyike vizuri zaidi huku akiwatoa wasiwasi
wananchi
kuwa shughuli za kimaendeleo na kijamii hazitaathiriwa na
kufanyika
kwa zoezi la Sensa kwakuwa zitaendelea kama kawaida.
Awali
Mratibu wa Sensa mkoa wa Mbeya Theresia Lyimo alisema mafunzo
hayo
yanahudhuriwa na washiriki 249 ambapo 244 kati yao wanatoka
wilaya
za mkoani hapa na watano ni kutoka mkoani.
No comments:
Post a Comment