MREMBO BORA WA MISS SINZA 2012 KUPATIKANA KESHO, TWANGA KUWASHA MOTO
MASHINDANO
ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012
yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten
Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.
Mashindano
hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho
pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda
ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali
ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya
Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo
atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/= katika mashindano hayo
yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’
ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa
vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa
akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
Akizungumza
na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy
Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs
400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi
wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata
sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha
Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa
warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo
watachuana ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi
atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi
yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti vya kawaida
na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina
yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza
wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema
Majuto.
Majuto
aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam
Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva
Mushi, Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano
hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa
Hotel, Clouds FM, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point,
Fredito Entertainment, Screen Masters, Lady Pepeta na flexi.
No comments:
Post a Comment