KAMATI
ya ulinzi na usalama wilayani Mbarali mkoani Mbeya imeagizwa kumsaka mganga wa
jadi anayetajwa kuwapotosha wananchi katika kata ya Ruiwa na kusababisha
kuwazika watuhumiwa wa uchawi wakiwa hai.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alitoa agizo hilo katika kikao
maalumu cha baraza la madiwani wilayani Mbarali kilicholenga kujadili taarifa
ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG).
Kandoro
alisema katika kata hiyo tayari yalitokea mauaji ya mkazi mmoja aliyezikwa kwa
kufukiwa kaburini akiwa hai na tukio la pili ilikuwa azikwe chifu wa eneo hilo
ajulikanaye kama chifu Merere lakini akaokolewa na askari wa jeshi la polisi.
Alisema
matukio ya mauaji hayo ynaelezwa kusababishwa na mganga mmoja wa jadi
aliyehamia kwenye kata hiyo akitokea wilayani Mbozi ambaye amekuwa akipiga
ramli na kuwatuhumu baadhi ya wakazi kuwa wasababishi wa vifo vya watu ndani ya
vijiji vya kata hiyo.
Kufuatia
maoni yam ganga huyo wakazi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi kwa
kuwazika hai watuhumiwa pasipo ushahidi wowote wa kisheria na wala maamuzi
kutoka vyombo vya dola.
Akizungumzia
hali hiyo mkuu wa mkoa alisema ni lazima kamati ya ulinzi imtafute mganga huyo
na kumkamata na kuhakikisha inampa taarifa haraka iwezekanavyo.
Alisema
jamii inahitaji amani na utulivu ili ijishughulishe na shughuli za kimaendeleo
hivyo kuwepo kwa mtu anayechochea upotevu wa amani hauwezi kuvumiliwa hivyo ni
lazima mganga huyo achukuliwe hatua.
Alisema
waganga kama hao hawahitajiki mkoani hapa kwakuwa badala ya kuisaidia jamii
kuondokana na matatizo wanasababisha migogoro inayowaingia wananchi katika hali
hataari kwa amani waliyo nayo.
No comments:
Post a Comment