Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 9, 2012

WAKANDARASI WAZAWA WAANZISHA CHAMA

WAKANDARASI wazawa nchini wameanzisha chama chao cha Tanzania Local Contractors Organization (TLCO) chenye lengo la kushughulikia changamoto zinazoikabili mipango ya utendaji kazi zao.

Mwenyekiti wa TLCO Kura Mayuma alikitambulisha chama hicho leo(Julai 8) kwa waandishi wa habari na kuthibitisha kuwa tayari kimesajiriwa na msajiri wa vyama vya hiari tangu Juni 26 mwaka huu na kupata cheti namba S.A.18225.

Mayuma amesema changamoto zinazowakabili wakandaarasi nchini ndizo zilipelekea wakae na kuona umuhimu wa kuwa na chombo kama hicho wakiamini kitakuwa na nguvu ya kweli ya kutatua matatizo yao.

Amesemaa chama hicho kitawaunganisha wakandarasi ili kupigania haki zao na kuwa na sauti moja ya kuiomba serikali iweze kuwathamini vya kutosha kama wazawa wanaotoa mchango mkubwa kwenye fani ya miuondombinu.

Amesema pia kitawawezesha weakandarasi wenyewe kuungana na kuweza kusaidiana wenyewe badala ya kuoneana wivu na kukosa mshikamano hivyo chama kitaweza kumaliza matatizo baina yao ama wao na waajiri kwa hatua za awali.

Ameongeza kuwa TLCO pia itapigania usawa kwenye upatikanaji wa kazi akisema kwa muda mrefu kumekuwepo na tatizo kubwa kwamba wakandarasi wazawa kunyimwa kazi na serikali yao kwa hisia na visingizio mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mitaji na kuwajali kwa kuwaamini zaidi wanaotoka nje.

No comments:

Post a Comment