Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, July 30, 2012

NI VURUGU,MGOMO,MAANDAMANO TUNDUMA

KUFUATIA Mgomo wa walimu ulioanza leo, wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi waliamua kuandamana ili kudai haki ya kufundishwa katika maandamano ambayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya mji wa Tunduma na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.

Hatua hiyo ilijitokeza mapema saa 2asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri wa Tunduma,walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani ambapo baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi cha mjini hapa kabla ya kufika ofisi za halmadhauri ya mji.

kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, awali wanafunzi hao walikwenda nyumbani kwa diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka (CHADEMA) na baada ya kufanya mazungumzo na mke wa diwani huyo ambaye inadaiwa hakuwepo waliandamana hadi kituo cha polisi na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya mji ambapo msafara huo uliingiliwa na baadhi ya watu walioendesha uporaji huo.


Mmoja wa Shuhuda hao ambaye alijitambulisha kuwa ni Julius Edward, alidai kuwa baada ya wanafunzi hao kufika katika ofisi  za polisi walipokelewa na kufanya mazungumzo ambayo  maamuzi yake hayakuafikiwa na wanafunzi hao.


Alisema baada ya kutoafiki majibu yaliyotolewa na Polisi
  wanafunzi hao waelekea kwenye mzunguko wa barabara uliopo karibu na eneo la ofisi za Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika mpaka wa Tanzania na Zambia ambako walizuia barabara ili magari yasipite.

Usumbufu huo ulidaiwa kujitokeza kwa muda wa nusu saa, hatua ambayo ilisababisha   polisi wa kituo hicho kufika eneo hilo na kulazimika
 kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia mabomu mawili ya machozi hali ambayo ilisababisha vibaka kujiingiza na kuaanza uporaji kwa kukimbilia ziliko ofisi za halmashauri ya mji.

Watu hao ambao wameonekana wakivamia ofisi hizo na kuchoma moto baadhi ya mali za halmashauri hiyo huku wakipora  kompyuta 5 za ofisi, pikipiki yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali sambamba na kuvunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya kubebea taka aina FAW  SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo  na gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.


Kulingana na tukio hilo vibaka wameweza kuonekana wakipora mali katika ofisi hizo huku wengine wakivunja chumba cha kuhifadhia mizigo mbalimbali na kufanikiwa kuiba mabati na viti na mali nyingi zilizokuwa zikibebwa,huku baadhi yao walionekana wamebeba madumu ya mafuta ya petroli wakitishia kuchoma jengo hilo.


Aidha Wanacnhi wa mjini hapa wanakumbuka matukio mbalimbali yanayojitokeza katika mji huu kuwa huwa yana leta adhari, kama ilivyo tokea katika matukio machache ya Februari 18, 2005 kufuatia wamachinga watano waliokamatwa Nakonde Zambia na mnao Septemba mosi hadi 3 mtu mmoja aliyefia  katika mahabusu ya Nakonde nchini Zambia.


Mji wa Tunduma umekuwa kinala cha  matukio ya vurugu  na uvunjifu wa amani linapotokea jambo lolote hali ambayo huchangiwa na
  watu wanaojiita wana harakati kuongoza vikundi vya watu ambao huaribu na kupora mali za watu.

Mkurugenzi wa mji huu Aidan Mwanshiga alipotakiwa kuelezea uharibifu hu alisema kuwa
  tadhimini ya uharibifu uliotokea inafanywa na taarifa rasmi itatolewa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akizungumzia tukio hilo alisema kuwa tukio hilo haliwezi kuvumiliwa kutokana na kuwa maandamano ya wanafunzi hayawezi kupelekea kuvunjwa kwa ofisi za serikali bali kuna watu ambao wametumia mwanya huo ili kupora mali.

Aidha Kamanda Diwani alisema mbali ya uharibifu wa mali za Mamlika ya mji wa Tunduma hakuna madhala mengine yaliyotokea ikiwa ni pamoja na majeruhi au vifo vilivyojitokeza.


Wakati huo huo katika Kata ya Vwawa wanafunzi wa shule za Ichenjezya na Haloli waliandamana hadi ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mbozi na baada ya maandamano hayo walirejea shuleni kwao kwa amani huku wakisindikizwa na Polisi.

aidha wanafunzi hao walidai kuwa walimu wao walifika shuleni lakini hawakuwa tayari kufundisha wakiwaambia kuwa hawatafundisha kwa vile wapo kwenye mgomo hivyo waliwashauri waandamane hadi ofisi za halmashauri kudai haki yao hiyo.


Vilevile habari kutoaka Jijini Mbeya zimeeleza Mbeya zimeeleza kuwa mgomo ulianza mapema leo asubuhi, ambapo walimu walifika shuleni na kusaini kitabu cha mahudhurio kisha kukaa kimya huku wakiawaacha wanafunzi wakilandalanda bila cha kufanya.

No comments:

Post a Comment